Ruhusa ya kuweka mashindano ya kuhifadhi qurani

Ruhusa ya kuweka mashindano ya kuhifadhi qurani

سئلت اللجنة: هل يجوز أخذ جوائز مسابقات القرآن الكريم؟

Iliulizwa kamati ya kudumu ya kutoa fatwa ya Saudia:

Je, inaruhusiwa kuchukua zawadi za mashindano ya qurani?

فأجابت: لا حرج في أخذ الجوائز التي ترصدها الجماعات الخيرية ونحوهم ممن يعنون بتحفيظ كتاب الله

Basi (kamati) ikajibu: Hakuna ubaya wa kuchukua zawadi ambazo huziweka jumuia za kheri na mfano wa hizo katika wale wanaotilia umuhimu kuhifadhisha qurani.

“فتاوى اللجنة الدائمة” ( 189 / 15 )

Maelezo:

Inafaa kuweka mashindano ya qurani kama zifanyavyo jumuia na taasisi mbalimbali za kiislamu huweka mashindano na zawadi kwa ajili ya kuhamasisha watu kuhifadhi qurani haswa vijana na hii ndiyo kauli ya wanachuoni wetu kadhaa waliopita na wa sasa kama ibn l-Qayyim, na wasasa ibn Uthaimin – na hawa wanachuoni wa kamati ya fatawa ya kudumu ya Saudia na wengine wengi na wameeleza kuwa mashindano ya kuhifadhi qurani au ya kielimu kama kuhifadhi hadithi au fiqih n.k, ni katika jihadi kwa hiyo yanaingia katika kauli yake Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie-:

“لَا سبَقَ إلَِّا فيِ نصَلْ أوَ خفٍُّ أوَ حاَفرِ” {

Hakuna posho/zawadi isipokuwa katika (mashindano ya) kurusha silaha, au (mashindano ya) ngamia au farasi } Maana ya hadithi: Haifai kuchukua zawadi katika mashindano yasiyokuwa haya kwa sababu hivi vilivyotajwa, hutumika katika jihadi kwa hiyo ni maandalizi ya jihadi, na vile vile kunaingia kuhifadhi qurani na elimu kama hadithi na elimu nyingine za kisheria. Tanbihi: Ama wanaosema kuwa kuna watu wanashindana kwa sababu ya kutaka mali/Zawadi! hii si hoja ya msingi kwa sababu ikhlaswi na kutakasa nia hili halidhihiri, Bali lipo katika moyo wa mtu hatuwezi kukataza hili kwa sababu ya dhana hiyo, ila watu wahimizwe kuwa na ikhlaswi na kufanya mambo yao kwa ajili ya Allah haswa kukihifadhi kitabu cha Allah.

[1] ibn Uthaymin;

الباب المفتوح” ( 26 / 59 ) A-baabul-maftuuh (26/59)

[2] ibn l-Qayyim;

الفروسية” (ص 318 ) Al-furuusiyyah (ukurasa:318

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 20/ Jumaadal-ulaa, 1442H ≈ 04/ Jan, 2021M. Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Kupata faida nyingi jiunge nasi Telegram, bonyeza hapa : ⬇️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *