✍ يقول السائل: ما هي أسباب قسوة القلب، والعلاج من ذلك؟
Anasema muulizaji : Ni zipi sababu za ugumu wa moyo ,na tiba kutokana na hilo ?
✍ أجاب الشيخ ابن عثيمين رحمه الله تعالى -:
Akajibu sheikh ibn ‘Uthaimin- Allah aliyetukuka amrahamu-:
◾️ أسباب قسوة القلب:
Sababu za ugumu wa moyo :
⬅️ الإعراض عن الله -عز وجل- والبعد عن تلاوة القرآٓن، واشتغال الإنسان بالدنيا، وأن تكون الدنيا أكبر همه،
Kumpuuza Allah -aliyeshinda na kutukuka- na kujitenga mbali na kusoma qurani , na mwanadamu kujishughulisha na dunia, na kuwa dunia ndiyo makusudio yake makubwa zaidi ,
فلا يهتم بأمور دينه، لأن طاعة الله – تعالى – توجب لين القلب ورقته، ورجوعه إلى الله -تبارك وتعالى-.
Na (akawa) hatilii umuhimu mambo ya dini yake kwa sababu kumtii Allah- aliyetukuka- huwajibisha ulaini wa moyo na wepesi wake na kurejea kwake kwa Allah-aliyezidi heri na kutukuka
⬅️ ودواء ذلك بالإقبال على الله، والإنابة إليه، وكثرة ذكره، وكثرة قراءة القرآٓن، وكثرة الطاعات بحسب المستطاع.
Na dawa ya huo (moyo mgumu) ni kumuelekea Allah ,na kurejea kwake, na wingi wa kumtaja ,na wingi wa kusoma quran na wingi wa ibada kadri inayowezekana .
📚 فتاوى نور على الدرب المجلد ١٢ ص ١٨.
Maelezo ya mfasiri:
Tunamuomba Allah azilainishe nyoyo zetu, na inawajibika tujue kuwa ugumu wa moyo ni katika sababu za kuingia motoni, na imethibiti hadithi kutoka kwa Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- pindi alipotaja katika sifa za watu wa motoni akasema:
( كلُّ عُتُلٍّ جَوَّاظٍ مُستكبِرٍ)
(Kila mgumu (wa moyo), asiyekuwa na subira hata kidogo, mwenye kiburi) .
متفق عليه.
Na moyo utakapokuwa mgumu hauwezi kuathirika na maneno ya Allah -aliyetukuka- na wala maneno ya Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 24, 1443H ≈ Jan 27, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•