https://t.me/fawaidussalafiyatz
Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
SAHIHISHA UFAHAMU WAKO KATIKA AYA HII .
قال الشيخ ابن عثيمين رحمه الله :
قال تعالى :
{ فاتقوا الله ما استطعتم}
Amesema sheikh ibn ‘Uthaimin – Allah amrahamu-:
Amesema (Allah) aliyetukuka-:
{Mcheni Allah (kadri) muwezavyo}
وهذه الآية ليست آية يقصد بها التهاون بتقوى الله
← وإنما يقصد بها الحث على التقوى بقدر المستطاع
● أي : لاتدخر وسعاً في تقوى الله
Hii aya si aya inayokusudiwa kuzembea kumcha Allah ,na hakika si vinginevyo (aya hii) makusudio yake ni mahimizo ya kumcha (Allah) kadri inavyowezekana .
Maana yake : usizembee katika kumcha Allah .
ولكن الله لا يكلف الإنسان شيئاً لا يستطيعه
كما قال تعالى :
(لا يكلف الله نفساً إلا وسعها)
Lakini Allah hamkalifishi mwanadamu chochote asichokiweza ,kama alivyosema (Allah) aliyetukuka-:
{Allah haikalifishi nafsi yoyote ila yanayolingana sawa na uwezo wake }
المصـــدر :
[شرح رياض الصالحين (١\٥١٤)
Maelezo:
Kila mja ni wajibu amche Allah kadri ya uwezo wake kwa maana atoe juhudi zake zote katika kumcha Allah ,ndio maana Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- ameamrisha mtu akishindwa kuswali hali ya kusimama ataswali amekaa ,na akishindwa kuswali hali amekaa ataswali hali amelalia ubavu.
Na hivi hivi katika ibada zote anatakiwa mtu ajipinde vile anavyoweza na kadri ya uwezo wake wa mwisho .
Kwa hiyo ni katika ufahamu mbaya mtu kuacha kufanya mambo mbali mbali ya wajibu kisha akasema Allah anasema :
{Mcheni Allah (kadri) muwezavyo} .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 29, 1442H ≈ Jun 10, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•