Sharti za mwanamke kutoka nyumbani

قَـالَ ابْـنُ المُلَـقَّن رحمه الله

Amesema ibn Al-mulaqqan – Allah amrahamu

قَـالَ بَعْـضُ الحُكَـمَاءِ لَا تَخْـرُجُ المَـرْأَهُ إِلَّا بِخَـمْسَةِ شُـرُوطٍ

Wamesema baadhi ya wenye hekima: Mwanamke asitoke (nyumbani kwake) ila kwa sharti tano:

أَنْ يَكُونَ ذَلِكَ لِضَرُورَةٍ

أَنْ تَلْبِسَ أَدْنَى ثِيَابِهَا

أَنْ لَا يَظْهَرَ عَلَيْهَا الطِّيبْ وَمَا فِي مَعْنَاهَا مِنْ بَخُورٍ

أَنْ يَكُونَ خُرُوجُهَا فِي طَرَفَيْ النَّهَارِ

أَنْ تَمْشِي فِي طَرَفَيْ الطُّرُوقَاتِ دُونَ وَسَطِهَا لِئَلَّا تَخْتَلِطُ بِالرِّجَالِ

1 – Uwe (huo utokaji) ni wa dharura.

2 – Avae nguo yake dhalili zaidi.

3 – Kusidhihiri juu yake manukato na chenye maana ya hayo (manukato) kama vile udi.

4 – Uwe (utokaji wake) ni asubuhi na jioni.

5 – Atembee pembezoni mwa njia si katikati yake ili asichanganyike na wanaume.

الإِعْلاَم بِفَوَائِد عُمْدَة الأَحْكَام ٢٣٠/٢

Maelezo:

Sharti la kwanza: Mwanamke asitoke nyumbani kwake ila kwa dharura kwa sababu hii ndiyo asili ya mwanamke kama alivyosema Allah:

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ ۖ

{ Na kaeni katika majumba yenu na wala msidhihirishe mapambo kama walivyokuwa wakidhihirisha wanawake wa zama za ujinga }.

Mfano wa dharura ni kama vile mtoto anaumwa sana na hakuna wa kumpeleka hospital basi atoke kwa kufuata misingi ya kisheria na pia anaruhusiwa kutoka kwa haja kama vile kutembelea ndugu, majirani na kuhudhuria harusi ikiwa hakuna fitna na maovu na kwa kufuata vigezo vya kisheria.

Sharti la pili: Avae nguo dhalili kwa maana asivae nguo ya kujionesha na kujipambanua na wenzake kiasi ambacho kila anayemuona anamuona amepambanuka kwa vazi hilo na pia asivae nguo dhalili zaidi kama vile mbovu au iliyochanika chanika kiasi ambacho watu wakimuona wanamshangaa, na katika hili kuna makemeo kama alivyosema Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie:

مَنْ لَبِسَ ثَوْبَ شُهْرَةٍ فِي الدُّنْيَا أَلْبَسَهُ اللَّهُ ثَوْبَ مَذَلَّةٍ يَوْمَ الْقِيَامَةِ

{ Mwenye kuvaa vazi la umaarufu duniani Allah atamvisha vazi la udhalili siku ya kiama }

Kwa hiyo haifai kuvaa nguo ya kujionesha na kujipambanua ima kwa thamani yake ya juu au kwa udhalili wake kupita kiasi bali avae nguo yake ya kawaida.

Sharti la tatu: Asipake manukato anapotoka nyumbani au ikiwa hapo nyumbani kuna mwanaume anayeruhusiwa kumuoa yaani si mahramu wake, kwa sababu ni katika madhambi makubwa kama alivyosema Mtume – swala na salamu zimfikie-:

أَيُّمَا امْرَأَةٍ اسْتَعْطَرَتْ فَمَرَّتْ عَلَى قَوْمٍ لِيَجِدُوا رِيحَهَا فَهِيَ زَانِيَةٌ وَكُلُّ عَيْنٍ زَانِيَةٌ

{ Mwanamke yeyote aliyepaka manukato na akapita kwa watu matokeo yake ni wale (watu) watapata harufu yake, basi huyo (mwanamke) ni mzinifu na kila jicho (linalomtizama) ni lenye kuzini }

صحيح الجامع ٢٧.١

Sharti la nne: Atoke asubuhi mapema au jioni kwa sababu ni wakati ambao anakuwa haonekani vizuri muda huo utakuwa ni stara kwake.

Sharti la tano: Asitembee katikati ya njia kama ilivyokuja katika hadithi na kwa ajili ya kujitenga na wanaume, kama Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie alipowaambia wanawake pindi alipoona wamechanganyika na wanaume-:

اسْتَأْخِرْنَ فَإِنَّهُ لَيْسَ لَكُنَّ أَنْ تَحْقُقْنَ الطَّرِيقَ عَلَيْكُنَّ بِحَافَّاتِ الطَّرِيقِ

{ Jitengeni (na wanaume) na hakika hali ilivyo hamuruhusiwa kupita katikati ya njia, jilazimisheni (kupita) pembezoni mwa njia }

فَكَانَتْ الْمَرْأَةُ تَلْتَصِقُ بِالْجِدَارِ حَتَّى إِنَّ ثَوْبَهَا لَيَتَعَلَّقُ بِالْجِدَارِ مِنْ لُصُوقِهَا بِهِ

Basi alikuwa mwanamke (baada ya amri) akijishikamanisha na ukuta mpaka nguo yake ilikuwa ikinasiana na ukuta kutokana na kujigandisha kwake na ukuta.

رواه أبو داود رقم/٥٢٧٢

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 14 – Safar – 1442H ≈ 01 – October – 2020M.

Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *