SHARTI ZA UMRI WA VICHINJWA VYA UDH’HIYAH

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

شروط سن الأضحية،

MASHARTI YA MIAKA YA (VICHINJWA VYA) UDH’HIYAH

قال العلامة ابن عثيمين- رحمه الله- :

Amesema mwanachuoni mkubwa ibn ‘Uthaimin- Allah amrahamu-:

الأبل خمس سنين،
البقر سنتان،
المعز سنة،
الخروف ستة أشهر.

Ngamia (awe na) miaka mitano,
Ng’ombe (awe na) miaka miwili,
Mbuzi (awe na) mwaka mmoja,
Kondoo (awe na) miezi sita.

📚 فتاوى ابن عثيمين (٢٥/١٣)

[ Fatawa Ibn Uthaimin (13/25) ]

Maelezo ya mpitiaji tarjama:

Umri uliotajwa ni huo na kuendelea, lakini asiwe ni mwenye umri mkubwa sana, yaani asiwe ni mzee mpaka akakosa uroto katika mifupa yake na nyama yake ikawa ngumu na ladha yake si nzuri kutokana na kuzeeka kwake, huyu ni katika wanyama walio katazwa kuchinjwa udh’hiyah,

Kwa maana mnyama akizeeka sana huwa anakuwa hana uroto katika mifupa yake pia nyama yake huwa ngumu na ladha yake si nzuri basi huyu hafai kuwa kichinjo cha Udh’hiyah.

Faida:

Umri wa mbuzi na kondoo kuna tofauti ya wanachuoni na kauli aliyoitaja sheikh- Allah amrahamu- ni ya Hanabilah , ama katika madhehebu (ya kishafii) :
Mbuzi lazima atimize miaka miwili ,na kondoo ni lazima atimize mwaka mmoja ila kama kondoo akiwa meno yake ya mbele yametoka katika miezi hiyo sita basi atafaa kuchinjwa,na mara nyingi akifiki miezi sita hudondosha meno yake ya mbele .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Iliandaliwa:August 10,2019M ,ikatumwa tena Dhul-Qaadah 29, 1442H ≈ Jul 9, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *