SHEIKH ABDUL-QAADIR AL-JAILAANIY -ALLAH AMRAHAMU-

قال الشيخ صالح الفوزان- وفقه الله-

Amesema sheikh Swaalih l-fauzan-Allah amuafikishe:-

”عبد القادر الجيلاني – رحمه الله- ليس صوفيا وإنما هو إمام جليل من قدماء أئمة الحنابلة, والطريقة المنسوبة إليه مكذوبة عليه, وليست طريقة له

“Abdul-Qaadir Al-jailaaniy-Allah amrahamu- si sufi (mwanatwariqa)

Na bila shaka sivinginevyo huyo ni imamu mtukufu katika wakongwe wa maimamu wa Mahanaabilah (madhehebu ya Ahmad) na twariqah ya Qaadiriya inayonasibishwa kwake ameongopewa na wala si twariqah yake “

📚 REJEA:-⇊

نقض كتاب تحقيق المقال للفريح ص (١٣٦) حاشية(٣)

MAELEZO YA MTARJUMU- ALLAH AMHIFADHI-

Sheikh Abdul-Qaadir -Allah amrahamu- hakuwa mtu wa twariqa na wala hakuanzisha twariqa ya Qaadiriyyah, na wala hakuwafundisha watu wamuombe na kumtaka msaada kama wanavyomfanyia baadhi ya wale wanaojinasibisha naye , hakuwafundisha watu wake ushirikina na uzushi, kwa hiyo masufi walijue hili na waache kumbandika uwongo na wajue kuwa itikadi yake ilikuwa ni ya kisalafi, na yafuatayo ni baadhi ya maneno yake katika upande wa itikadi akithibitisha sifa za Allah, bila ya kupindua wala kubadilisha na wala kufananisha ,na wala kuacha kuthibitisha !:

((وهو بجهة العلو مستو على العرش محتو على الملك محيط علمه بالأشياء))

((Na huyo (Allah) yupo upande wa juu ,yupo juu ya Arshi, ufalme (wake) umekusanya (kila kitu) elimu yake imevizunguka vitu (vyote)

(الْغُنْيَة ص ٧١)

Na akasema :

((له يدان وكلتا يديه يمين))

(Allah) ana mikono miwili na mikono yake yote miwili ya (Allah) ni yenye baraka .))

[الغنية ص ٧٢

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 25 , 1443H ≈ Aug 23, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *