SIFA SITA KATIKA SWALA NI MIONGONI MWA ALAMA ZA UNAFIKI .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

SIFA SITA KATIKA SWALA NI MIONGONI MWA ALAMA ZA UNAFIKI .

✍️قال الإمام ابن القيِّم – رحمه الله -:

Amesema imamu ibn A-qayyim- Allah amrehemu-:

ست صفات في الصلاة من علامات النفاق :

Sifa sita katika swala ni miongoni mwa alama za unafiki :

الكسل عند القيام إليها
ومراءاة الناس في فعلها
وتأخيرها

1-Uvivu wakati wa kuiendea,

2-Kuwaonesha watu (wakati wa) kuitekeleza .

3- Kuichelewesha.

ونقرها
وقلة ذكر الله فيها
والتخلف عن جماعتها.

4- Kuidonoadonoa (kuswali kwa haraka)

5- Uchache wa kumtaja Allah katika (hiyo swala)

6-Kujiepusha na jamaa.

المصدر : الصلاة وأحكام تاركها صـ١٢٣ ✍️

Maelezo ya mpitiaji:

Hizi ni miongoni mwa sifa za wanafiki katika swala yaani unafiki wa kiitikadi au unafiki mkubwa ambao unamtoa mtu katika uislamu na kuwa kafiri ,na miongoni mwa hizi sifa amezitaja Allah katika kitabu chake pale aliposema:

إِنَّ ٱلْمُنَٰفِقِينَ يُخَٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَهُوَ خَٰدِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوٓاْ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ قَامُواْ كُسَالَىٰ يُرَآءُونَ ٱلنَّاسَ وَلَا يَذْكُرُونَ ٱللَّهَ إِلَّا قَلِيلًا

Hakika wanafiki wanamkhadaa Allah ,na hali yeye (Allah) ni mwenye kuwakhadaa wao.Na wanaposimama kuswali husimama kwa uvivu ,wanawaonesha watu (kuwa wanaswali) wala hawamtaji Allah ila kidogo .

النساء : ١٤٢

Ufafanuzi wa aya:

Allah anaeleza kuwa wanafiki wanamfanyia khadaa Allah kwa kule kudhihirisha kwao uislamu na kuficha ukafiri , na yeye Allah -aliyetukuka- anawalipa khadaa yao kwa kuwakhadaa kwa kuwapa muda wa kuishi na kuendelea na kudhihirisha uislamu na kuficha ukafiri mpaka pale ambapo Allah atazitoa roho zao na hali wapo katika unafiki wao .

Na katika kawaida za wanafiki huwa hawana uchangamfu katika swala ,huiendea swala kwa uvivu na wanaposwali hawaswali kwa ajili ya Allah bali huwaonesha watu kuwa wao ni waislamu , na pia katika hizo swala hawamtaji Allah isipokuwa kidogo mno .

Na pia katika sifa za wanafiki ni kuchelewesha swala na kuswali haraka haraka kama ilivyosimulia Anas- Allah amridhie- kutoka kwa Mtume – swala na salamu zimfikie – kwamba amesema:

  • ألَا أُخبِرُكم بصَلاةِ المُنافقِ، يَرقُبُ الشَّمسَ حتى إذا اصفَرَّتْ فكانتْ بيْنَ قَرنَيِ الشَّيطانِ،

Je, hivi nikujulisheni swala ya mnafiki (ni hii) : Analingojea jua mpaka litapokuwa la njano likawa baina ya pembe mbili za Shetani

قام فنَقَرَ أربعًا لا يَذكُرُ اللهَ عزَّ وجلَّ فيها إلَّا قَليلًا.

(ukifika muda huo) husimama na huzidonoa (hizo rakaa) nne na wala hamtaji Allah ndani ya hiyo (swala) isipokuwa kidogo tu .

سنن الدارقطني

Maana ya hadith:

Mnafiki huchelewesha swala bila ya udhuru wa kisheria ,hulisubiria jua mpaka linapokaribia kuzama ni katika muda ambao Shetani hulielekea jua kwa pembe zake kama walivyoeleza wanawavyuoni , yeye huyo mnafiki huswali hizo rakaa nne haraka haraka kama vile ndege anavyodonoa punje za nafaka .

Sifa ya mwisho aliyoitaja ni kuacha kuhudhuria swala ya jamaa na kama akihudhuria basi huhudhuria kwa maslahi fulani kama kujionesha n.k.

Mwisho: Yeyote mwenye sifa miongoni mwa sifa hizi basi ajirekebishe kwa kuiacha sifa hiyo kwa sababu yupo katika hatari kubwa.

Mpitiaji:Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 7, 1443H ≈ October 13, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

1 Comment

  1. Eliyas

    Xhukran kwa wote wanaotufahamixha mambo haya ya kheri inxhallah mungu awafungulie akili zao zaidi ili watujulixhe na mengi zaid

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *