SIKUKUU YA WAPENDANDO (VALENTINE’S DAY)

من الأعياد الوثنية النصرانية فلا يحل لمسلم يؤمن بالله واليوم الآخر أن يفعله أو أن يقره أو يهنئ به

Ni katika sikukuu za kishirikina za kinaswara (kikristo) basi si halali kwa muislamu aliye muamini Allah na siku ya mwisho kuisherehekea au kuikubali au kutoa pongezi kwa (sikukuu) hiyo

بل الواجب تركه واجتنابه استجابة لله ورسوله وبعدا عن أسباب سخط الله وعقوبته،

Bali inawajibika kuiacha (hii sikukuu) na kujiepusha nayo kwa kujibu (amri) ya Allah na mtume wake na kujitenga mbali na sababu za kukasirikiwa na Allah na (kufikiwa) na adhabu zake

كما يحرم على المسلم الإعانة على هذا العيد أو غبره من الأعياد المحرمة

kama inavyo haramishwa juu ya muislamu kusaidia katika sikukuu hii au nyinginezo katika sikukuu zilizo haramishwa

بأي شيئ من أكل أو شرب أو بيع أو شراء أو صناعة أو هدية أو مراسلة أو إعلان أو غير ذلك

(Haifai kusaidia) kwa kitu chochote katika kula au kunywa au kuuza au kununua au kutengeneza (kitu) au kwa zawadi au kwa kutumiana massage (kutoa) tangazo au mengineyo yasiyo kuwa hayo

لأن ذلك كله من التعاون على الإثم والعدوان ومعصية الله ورسوله.

Kwa sababu hayo yote ni katika kusaidiana juu ya madhambi na uadui na kumuasi Allah na mtume wake.

المصدر: اللجنة الدائمة- المجموعة الثانية- (٢٦٢/٢)

MAELEZO YA MFASIRI

Haifai kusherehekea sikukuu yoyote ya kikafiri au ya kishirikina au ya kizushi na haifai kushiriki kwa namna yoyote katika sikukuu hizi:

Kama vile kuandaa chakula maalum, au vinywaji au kuvaa mavazi maalumu kwa ajili ya sikukuu hii pia kama mfanya biashara haifai kuuza vitu ambavyo maalum hutumika katika sikukuu hizi

kama vile kuuza maua mekundu ,mavazi mekundu n.k, na kama ni fundi ni haramu kushonesha mavazi yatakayotumika kusherekea siku kuu hizi, pia ni haramu kutoa pongezi kwa ajili ya sikukuu hizi

Na pia kutuma sms za kuadhimisha sikukuu hizi yote haya ni haramu, na hata kukubali na kukiri kwamba hiyo ni sikukuu

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imerushwa kwa mara ya tatu : Mfungo kumi 12, 1443H ≈ Feb 13, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *