🌴عن عمر بن الخطاب – رضِيَ الله عنه أنه قال -:
Amesema Umar bin Al-khattwab- Allah amridhie-:
إنّ أفضل عيش أدركناهُ بِالصّبر، ولو أنّ الصّبْرَ كانَ من الرِّجال كان كريماً.
Bila shaka maisha bora (tuliyoyapata) tumeyapata kwa subira ,na lau subira ingekuwa ni katika watu (basi) angekuwa ni (mtu) mwenye mwema.
📚الصبر لابن أبي الدنيا ص٢٣
🍃🍂🍃🍂🍃🍂🍃🍂
Maelezo:
Kuwa na subira ni katika sababu za kuishi maisha mazuri yenye raha na utulivu ,na subira ni ibada mzito mno na ni nadra kupatikana kwa watu kama unavyoona kuwa watu wema na wakarimu ni wachache basi subira nayo ingekuwa ni katika watu basi ni sawa na mtu mwema ,mkarimu.