Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
🔹سنّــة مهجــورة
Suna iliyohamwa :
KUWEKA VIDOLE MASIKIONI WAKATI UNAPOSIKIA SAUTI YA ZUMARI /MUZIKI NA MFANO WA HIVYO .
يَقُولُ نَافٍعٌ مَوْلَى بن عمر – رضي الله عنهما –
Anasema Naafi’i aliyekuwa mtumwa wa ibn Umar- Allah awaridhie wawili hao-
سمع ابنُ عمرَ مزمارًا فوضع أُصبعَيه على أُذُنَيه ونأَى عن الطريق ِ
(siku moja) ibn Umar alisikia (sauti ya) zumari basi muda huo huo akaweka vidole vyake viwili masikioni mwake na akawajiweka mbali na njia (hiyo)
وقَـاَل لي يا نافعُ هل تسمع شيئًا..؟
فقلتُ: لا..
na akaniambia : Ewe Naafi’i je unasikia (sauti) hata kidogo ?
nikasema : Hapana (sisikii).
قـال : فرفع أصبعَيه من أُذُنَيه.
Akasema (Naafi’i) : basi akaondoa vidole vyake viwili katika masikioni yake
وقـال : كنتُ مع النبيِّ – صلى الله عليه وسلم –
فسمع مثلَ هذا فصنعَ مثل هذا.
na akasema: Nilikuwa pamoja na Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- na akasia mfano wa (sauti) hii ,basi akafanya kama hivi!!
صححه الشيخ الألباني – رحمه اللّه –
📚 [ تحريم آلات الطرب (١١٦)
Maelezo ya mtarjumu:
Maswahaba -Allah awaridhie- walikuwa na pupa ya kumfuata Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- na ibn Umar- Allah amridhie- alikuwa ni zaidi katika wao.
Pia katika hadithi kuna makemeo ya kupuliza mazumari na kusikiliza sauti ya mazumari na muziki ndiyo kabisa ,lakini ni ipi hukumu ya kupanda basi lenye muziki, na abiria akawa anasikia muziki bila ya kupenda ?
Tusome fatwa ifuatayo ya wanachuoni ili kufahamu jibu lake:
السؤال الثالث من الفتوى رقم (١٧٦٤١)
Swali la tatu kutoka katika fatwa namba (17641)
س ٣: نضطر إلى سماع الأغاني أو الموسيقى، سواء في الحافلة التي تنقلنا إلى العمل يوميا، أو الحافلات والتاكسيات التي نحتاجها في السفر بعض الأحيان، فما الحكم؟
Swali 3 : Tunapata dharula ya kusikia nyimbo au muziki sawa sawa katika basi ambalo linatupeleka kazini kila siku au mabasi na taxi ambazo tunazihitajia katika safari baadhi ya nyakati ,basi ni ipi hukumu ya (hili) ?
ج٣: إذا كنت لا تستطيع منع الأغاني في الحافلة وأنت محتاج إلى ركوبها لبعد المسافة،
Jawabu 3: Ukiwa huwezi kuzuia nyimbo/muziki ndani ya basi na wewe ni mwenye kuhitajia kupanda hilo (basi) kwa sababu ya umbali wa masafa,
ولا تجد وسيلة غيرها- فلا بأس عليك في ذلك، مع إنكار المنكر حسب استطاعتك، ولو في قلبك.
na ukawa haupati njia (nyingine ya kufika) isipokuwa hiyo ,basi hakuna ubaya juu yako katika hilo (lakini upande) pamoja na kupinga uovu kadri ya uwezo wako japo katika moyo wako (kwa kuchukia).
وبالله التوفيق، وصلى الله على نبينا محمد وآله وصحبه وسلم.
(Tumejibu) kwa taufiq ya Allah,na swala na salamu za Allah zimfikie Mtume wetu Muhammad na jamaa zake maswahaba wake .
اللجنة الدائمة للبحوث العلمية والإفتاء
Kamati ya kudumu ya utafiti wa kielimu na fatwa.
الرئيس: عبد العزيز بن عبد الله بن باز
عضو: صالح الفوزان
عضو: عبد العزيز آل الشيخ
Kiongozi: Abdul-Aziz bin Abdill bin Baz .
Kiungo: Swaleh Al-Fauzan.
Kiungo: Abdul-Aziz Alu-Sheikh .
Mtarjumu: Ismail Seiph Mbonde.
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Muharram/Mfungo nne 9, 1443H ≈ September 16, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•