سلسلة أحكام الصلاة.
MLOLONGO (MFULULIZO) WA HUKUMU ZA SWALA (NO. 67)
SWALA YA ISTIKHARA: SEHEMU YA PILI [2]
لماذا نصلي صلاة الاستخارة؟
Kwa nini tunaswali swala ya Istikhara?
قال الشيخ محمد بن عمر بن سالم بازمول – حفظه الله-:
Amesema Sheikh Muhammad bin Umar bin Salim Baazamuul – Allah amuhifadhi-:
شرع الرسول صلى الله عليه وسلم – لأمته أن يستعلموا الله ما عنده في الأمور التي تمر بهم في حياتهم، وأن يطلبوه تعالى الخيرة فيها وذلك بأن علمهم صلاة الاستخارة.
مكان ما كان يفعل في الجاهلية من الطيرة والاستسقام بالأزلام والقداح.
Ameuwekea Mtume – swala na salamu zimfikie – umati wake wamfahamishe Allah kwa kile kilichopo kwake katika mambo yanayowapitia maishani mwao na wamtake (Allah) aliyetukuka la heri katika hayo na hilo ni kwa kuwafundisha swala ya Istikhara.
(imewekwa Istikhara) nafasi ya yale yaliyokuwa yakifanywa katika (zama) za ujinga ambayo ni uchuro na kutezamia kwa kutumia mishale na upinde.
انظر: بغية المتطوع في صلاة التطوع لمحمد بازمول، ص: ١.٣
Angalia: Bughyatu l-mutatwwi’i fii swalaati ttatwwu’i cha Muhammad Baazamuul, ukarasa: 103
Maelezo:
Watu wa zama za ujinga kabla ya Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – walikuwa wanapotaka kufanya mambo yao hutegemea ishara ya vitu fulani kama ndege! Mfano mmoja wao anapotaka kusafiri humtimua ndege na anaporuka kwa kuelekea upande wa kulia hii ni ishara ya kuwa safari ni nzuri na anapoelekea upande wa kushoto ni ishara kuwa safari haina heri. Na wengine hutizamia /hupiga ramli kwa kutumia mishale na vitu vingine mbalimbali, uislamu ulipokuja uliyakataza haya na kuweka mbadala wa hayo ambayo ni swala ya kumuomba Allah akuchagulie lenye heri katika hayo mawili anayotaka kuyafanya. Itaendelea in shaa Allah, Usikose sehemu ya tatu [3].
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 05/ Jumaadal-aakhir 1442H ≈ 18/ Jan, 2021M.
Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⬇️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•