سلسلة أحكام الصلاة.
MLOLONGO (MFULULIZO) WA HUKUMU ZA SWALA (NO. 70)
SWALA YA ISTIKHARA: SEHEMU YA TANO [5]
أيهما يقدم: الاسْتِخَارَةِ أم الاستشارة؟
Kipi kinatangulizwa: Istikharah au kuomba ushauri?
Wanachuoni wametofautiana katika hili kuna wanaosema aanze kuomba ushauri kabla ya istikhara kama anavyosema Annawawiy – Allah amrahamu-:
” يُسْتَحَبُّ أَنْ يَسْتَشِيرَ قَبْلَ الاسْتِخَارَةِ مَنْ يَعْلَمُ مِنْ حَالِهِ النَّصِيحَةَ وَالشَّفَقَةَ وَالْخِبْرَةَ,وَيَثِقُ بِدِينِهِ وَمَعْرِفَتِهِ
Inapendeza kuomba ushauri kabla ya istikhara (atamtaka ushauri) yule anayeijua katika hali yake ni kutoa nasaha na huruma na uzoefu na anamuamini kwa dini yake na utambuzi wake
Amesema (Allah) aliyetukuka: “Na watake ushauri katika mambo”
قَالَ تَعَالَى: “وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ”
وَإِذَا اسْتَشَارَ وَظَهَرَ أَنَّهُ مَصْلَحَةٌ اسْتَخَارَ اللَّهَ تَعَالَى فِي ذَلِكَ.
Na atapotaka ushauri na kukamdhihirikia kuwa hilo (jambo lina) maslahi atamuomba Allah – aliyetukuka – amchagulie la heri katika hilo.
انظر: رياص الصالحين
Angalia: Riyadhu sswaalihiinsswaalihiin
Maelezo: Wanaosema kuwa anaanza kuomba ushauri kwanza kabla ya istikhara kama imamu Nnawawiy – Allah amrahamu – kwa sababu istikhara ni hatua ya mwisho yaani baada ya istikhar / baada ya kumuomba Allah akuchagulie lililo la heri basi unalifanya lile ulilolikusudia. Ama wale waliosema anaanza istikhara kabla ya kutaka ushauri kama Sheikh ibn ‘Uthaimin – Allah amrahamu – maelezo ni haya yafuatayo, Amesema Sheikh Muhammad bin Swaalih Al-‘uthaimin – Allah amrahamu-:
وقد اختلف العلماء: هل المقدم المشورة أو الاستخارة؟
Na bila shaka wametofautiana wanachuoni je, kunatangulizwa kuomba ushauri au istikhara?
والصحيح أن المقدم الاستخارة، فقدم ـ أولا ـ الاستخارة، لقول النبي صلى الله عليه وسلم: إذا هم أحدكم بالأمر فليصل ركعتين، إلى آخره. ثم إذا كررتها ثلاث مرات ولم يتبين لك الأمر فاستشر ثم ما أشير عليك به فخذ به وإنما قلنا إنه يستخير ثلاث مرات لأن من عادة النبي صلى الله عليه وسلم أنه إذا دعا دعا ثلاثا والاستخارة دعاء وقد لا يتبين للإنسان خير الأمرين من أول مرة بل قد يتبين في أول مرة أو في الثانية أو في الثالثة وإذا لم يتبين فليستشر.
Na sahihi ni kuwa linalotangulizwa ni istikhara, basi tanguliza – kwanza – istikhara, Kwa kauli yake Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie: “Pindi mmoja wenu atakapokusudia jambo basi aswali rakaa mbili ” mpaka mwisho wa hadithi. Kisha pindi atakapoirudia mara tatu na ukawa haukubainikiwa na jambo, basi taka ushauri, kisha utakaloashiriwa lichukue (lifanyie kazi), na hakika si vinginevyo tumesema: bila shaka ataleta istikhara mara tatu, kwa sababu katika kawaida ya Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – kuwa yeye anapoomba dua huomba mara tatu, na istikhara ni dua na huwenda kusimbainikie mwanadamu jambo la heri katika hayo mawili mwanzoni mwa jambo lake, bali huwenda likabainika mara ya kwanza au mara ya pili au ya tatu na kama haikubainikiwa basi aombe ushauri.
شرح رياص الصالحين
Sher’he ya riyadhi sswalihiin.
Ufafanuzi: Sheikh ibn ‘Uthaimin – Allah amrahamu – yeye anaona kuwa kwanza muislamu anatakiwa atangulize istikhara kabla ya kuomba ushauri na ndiyo kauli iliyokuwa sahihi kwa sababu Kumuomba Allah akuongoze katika jambo fulani kunatangulizwa juu ya kumuomba kiumbe kwa kumtaka ushauri.
Itaendelea in shaa Allah, Usikose sehemu ya tano [6].
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 19/ Jumaadal-aakhir 1442H ≈ 01/ Jan, 2021M.
Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⬇️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•