TABIA HII HUZINGATIWA NI KATIKA KUWAASI WAZAZI !

قَالَ عُرْوَةُ بْنُ الزُّبير رحمه الله:

Amesema ‘Urwah bin Azzubair-Allah amrahamu-:

” مَا بَرَّ وَالِدَهُ مَنْ شَدَّ الطَّرفَ إِلَيْهِ” .

Hakumfanyia wema mzazi wake, yule aliyemkazia macho huyo (mzazi wake) .

المصدر : سير أعلام النبلاء للذهبي 433/4

Maelezo ya mfasiri:

Kumtezama mzazi wako kwa jicho la hasira au la dharau au kumkazia macho, haya yote yanazingatiwa ni katika kuwaasi wazazi wawili ,na hapa ametajwa baba, lakini na mama pia na tena mama ndiye mwenye haki kubwa zaidi ya kufanyiwa wema kama alivyosema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- pindi alipoulizwa, ni nani mtu mwenye haki ya kuishi naye kwa wema zaidi ?,na Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -akamjibu:

أمك ثم أمك ثم أمك ثم أباك

Mama yako kisha mama yako kisha mama yako kisha baba yako .

متفق عليه .

Hapa utaona kuwa mama anamzidi baba mara tatu ,ni kwa sababu kuna mambo matatu ambayo ni mama pekee amepwekeka nayo na amepata tabu na shida, bila ya kushirikiana na baba nayo ni :

1-Kubeba mimba

2- Maumivu ya kujifungua

3- Kunyonyesha .

Ndiyo, baba naye anahaki kubwa ya kufanyiwa wema kwani yeye ndiye sababu ya kupatikana mtoto na yeye ndiye anayetoa huduma mbalimbali na anapata tabu katika hilo lakini ifahamike kuwa mama amepata tabu zaidi katika mambo yale matatu .

ربّ اغفرلي ولوالدي وارحمهما كما ربياني صغيرا
•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa : Mfungo mosi 4 , 1445H =Apr 13, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
    •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *