ذكر ابن كثير رحمه الله: أن شيخ الإسلام لما ألف كتابه ” الاستغاثة”
Ametaja ibn Kathir -Allah amrahamu- kuwa sheikh l-islam pindi alipotunga kitabu chake ” Al-istighathah”
ترصد له ابن البكرى الصوفى على الطريق ومعه جماعة من أصحابه وضربوا شيخ الإسلام ضربًا شديدًا حتى طرحوه على الأرض ثم هربوا..
Ibn Bakry Sufiy alimvizia (ibn Taimiyyah) njiani akiwa pamoja na kundi katika watu wake wakampiga sheikh l-islam kipigo kikubwa mpaka wakamuangusha ardhini kisha wakakimbia..
تجمع الناس بعدها ومعهم الجند وطلبوا من شيخ الإسلام أن يأذن لهم بالانتقام من ابن البكرى فرفض شيخ الإسلام وقال لهم :
Watu walikusanyika baada ya hilo (tukio) wakiwa pamoja na jeshi na wakamtaka sheikh l-islam awape idhini ya kulipiza kisasi kwa ibn Bakry, basi sheikh l-islam akakataa na akawaambia:
” إما أن يكون الحق لى أو لكم أو لله؛ فإن كان لي فهو فى حلٍّ وإن كان لكم؛ فإن لم تسمعوا منى فلا تستفتونى، وافعلوا ما شئتم وإن كان لله، فالله يأخذ حقه كيف شاء متى شاء “..
Ima haki (inaweza) ikawa ni yangu au yenu au ya Allah, basi kama (haki) ni yangu basi (ibn Bakry) nimemsamehe, na kama haki itakuwa ni yenu basi kama hamtonisikiliza (katika hili) basi msinitake fatwa (tena) na fanyeni mnalolitaka , na kama (haki) ni ya Allah basi Allah atachukua haki yake namna anavyotaka na muda anaotaka “
لكنهم لم يكترثوا بكلام شيخ الإسلام وسعوا فى طلب ابن البكرى فى كل مكان ..
Lakini hao (watu) hawakujali maneno ya sheikh l-islam na wakafanya juhudi katika kumtafuta ibn Bakry kila sehemu ..
لم يجد ابن البكرى مكانا يختبئ فيه إلا بيت شيخ الإسلام..
أواه شيخ الإسلام وخبأه حتى يشفع له عند السلطان فيعفو عنه..وقد فعل
Na ibn Bakry hakupata sehemu ya kujificha isipokuwa nyumbani kwa sheikh l-islam, (na) sheikh l-islam alimpokea na akamficha ili akamuombee kwa mfalme amsamehe , na hakika (ibn Taimiyyah) alilifanya hilo.
وهذا الموقف العجيب جعل بعض علماء الاشاعرة يقولون عن شيخ الإسلام :
Msimamo huu wa ajabu uliwafanya baadhi ya wanayuoni wa kiasha’ira wakisema:
تخلق بأخلاق لا تكاد تحصل إلا لأنبياء الله تعالى وأفراد الناس.
(Huyu ibn Taimiyyah) amejipamba na tabia (ambazo) zinakaribia kutopatikana isipokuwa kwa Manabii wa Allah aliyetukuka na watu mmoja mmoja
رحم الله شيخ الإسلام ابن تيمية.
Allah amrahamu sheikh l-islam ibn Taimiyyah .
البداية والنهاية (١٤/٧٦)، وذيل طبقات الحنابلة (٢/٤٠٠)، والعقود الدرية (ص٢٨٦)، والكواكب الدرية (ص١٣٩)
Maelezo ya mfasiri:
Bila shaka hizi ni katika tabia mzuri za kipekee ambazo wengi mno hatuna, tabia ambazo hata adui amezikiri kwa uzuri wake,
na bila shaka adui kawaida hutaja aibu na mapungufu ya yule anayemfanyia uadui lakini pindi atakapoona adui anataja sifa za yule anayemfanyia uadui basi tambua kuwa huyo anayefanyiwa uadui ana sifa ambazo hakuna wa kuzipinga hata maadui wake wanazikiri, na hili ndilo lilotokea kwa ibn Taimiyyah -Allah amrahamu- sifa zake wamezikiri hata maadui wake, na kama tulivyosema ukiona mtu anasifiwa hata na adui wake basi tambua kuwa huyo mtu ana ubora wa kipekee, kama alivyosema mshairi pale alipomsifu yule aliyemsifa:
وشمائلٌ شهِد العدو بفضلها
Na sifa (mzuri ambazo) adui ametoa ushahidi kwa ubora wake.
والفضل ما شهدت به الأعداء
Na ubora ni (ule) alioutolea ushahidi adui.
Tanbih:
Hivi ndivyo wanavyuoni walivyo huyafanya mambo yao kwa elimu ,na kwa kuangalia faida na madhara na wala hawafanyi mambo kwa kukurupuka kama wafanyavyo wajinga !
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 9, 1443H ≈ Jan 12, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•