يقول العلامة ابنُ قيم
الجوزية-رحمهُ اللهُ- :
Anasema mwanachuoni mkubwa ibn l-Qayyim -Allah amrahamu-:
((ومِنَ النَّاسِ مَنْ طَبْعهُ طبعُ خِنزيرٍ ، يَمُرُّ بالطيباتِ فلا يَلْوي عليها ،
Na miongoni mwa watu kuna yule ambaye tabia yake ni tabia ya nguruwe,huvipita (vyakula) vizuri bila ya kugeuza (shingo yake),
فَإِذا قامَ الإنسانْ عنْ رَجيعهِ قَمَّهُ ،
na pindi mwanadamu anaposimama baada ya kumaliza kujisaidia hukivamia na hukila hicho (kinyesi) chote,
وهَكَذا كثيرٌ منَ النَّاسِ يَسمعُ مِنكَ ، ويَرى منَ المحاسنِ أضعافَ أضعافِ المساوىء ؛
na hivi hivi ndivyo (walivyo) wengi katika watu husikia kwako na huona katika mema zaidi na zaidi ya mabaya
فَلا يحفظُها ، وَلا يَنْقُلُها ، ولا تُناسِبُه ؛
hayahifadhi na wala hayahamishi na wala hayamfai,
فَإذا رَأى سَقطةً ، أَوْ كَلمةً عوراءَ :
na pindi alionapo kosa au neno baya :
وَجَدَ بُغيتَهُ وما يُناسِبُها ، فَجَعلها فَاكهتَهُ ونُقْلَهُ))
(hapo sasa) hupata kile anachokitafuta na huyafanya haya (makosa) ndiyo kiburudisho chake na ndiyo maneno yake ya kuyasambaza.
مدارج السالكين (406/1)
Maelezo ya mfasiri:
Hii ni tabia ya nguruwe na kuna baadhi ya watu wanatabia kama hii.
Nguruwe yeye kwa ule uchafu aliokuwa nao huwa hana haja na vyakula vizuri٫ isipokuwa anapomuona mwanadamu amejisaidia sehemu fulani haja kubwa, yeye haraka hukivamia hicho kinyesi na kukila chote na hivi ndivyo walivyo baadhi ya wanadamu huwenda wakayaona mema mengi kwa mtu ambaye muonekano wake ni wa wema , na mabaya yake ni machache lakini hawa watu kwa sababu ya uchafu wa nyoyo zao ,haya mema hawayahifadhi na wala hawayasambazi kwa watu na huona kuwa haya mema hayawafai !lakini watu hawa pindi wanapoliona kosa au neno baya huyachukua makosa haya na kuyasambaza, na huyafanya makosa hayo kuwa ni mazungumzo ya vikao vyao ,na yote haya ni kwa sababu wao lengo lao ni kupekua makosa tu na kuyaacha mema ya mwema huyu !
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 8, 1445H ≈ Dec 21, 2023M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•