Tafsiri na faida

قال تعالى

Amesema (Allah) – aliyetukuka-:

هو أعلم بكم إذ أنشأكم من الأرض

سورة النجم

{ Yeye anawajua zaidi nyinyi pindi alipowaumba kutokana na ardhi (alipomuumba Adamu) }

قال الشيخ ابن عثيمين رحمه الله في تفسيره لهذه الآية

Amesema Sheikh ibn ‘Uthaimin – Allah amrahamu – katika tafsiri ya aya hii

‏ولذلك الآن بنو آدم كالأرض تماما فيهم الحزم الصلب الشديد وفيهم السهل وفيهم ما بين ذلك ‏وفيهم الأبيض وفيهم الأحمر وفيهم الأسود لأن الأراضي تختلف هكذا

Kwa ajili hiyo hivi sasa wanadamu (wapo) kama ardhi sawa sawa, katika hao (wanadamu) kuna wagumu wakali na katika hao kuna wepesi na katika hao kuna wale baina ya hao na katika hao kuna weupe na katika hao kuna wekundu na katika hao kuna weusi, kwa sababu ardhi inatofautiana hivi.

تفسير القرآن ٢٣٦/٤

Maelezo: Yaani tabia za wanadamu zinatofautiana kama zinavyotofautiana sehemu za ardhi kuna nyekundu, nyeusi n.k, na pia kuna sehemu laini na ngumu, na hivi ndivyo tulivyo katika dunia kuna waumini na makafiri. Na Allah – aliyetukuka – anatujua zaidi kuliko tunavyozijua nafsi zetu. Fuatilia makala inayofuata upate ufafanuzi zaidi.

Mfasiri: fawaidusalafiya.net Imeandaliwa: Tarehe 10 – Safar – 1442H ≈ 27 – September – 2020M.

Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz

Muhimu: Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *