قال الشيخ سليمان الرحيلي -حفظه الله- :
Amesema sheikh Suleiman Arruhailiy – Allah amuhifadhi-:
🟥 أنانة: هي كثيرة الأنين و الشكوى لا ترضى بشئ و لا يعجبها شئ و لا تكاد تكون مرتاحة مع زوجها، هذه لا تطيب معها الحياة .
Mwingi wa kuugulia : Huyo ni yule (mwanamke ambaye ni ) mwingi wa kuugulia na malalamiko, haridhii chochote na wala hakimpendezi chochote na anakaribia kutokuwa na furaha na mumewe , (mwanamke) huyu maisha hayawi mazuri pamoja naye.
🟧حنانة: هي التي تحن إلى زوج آخر و تمتن على زوجها بنفسها، و تقول مثلي يكون لمثلك … مثلي يتزوجها كذا و كذا.
Mwingi wa shauku :Huyo ni yule (mwanamke ambaye) anashauku ya mume mwingine na anajifadhilisha juu ya mumewe, na husema : (Hivi) mfano wa mimi naweza nikawa (mke) wa mfano wako …mfano wangu mimi huolewa na (mtu) kadhaa wa kadhaa
🟨حداقة: هي التي ترمي بعينها في كل شئ و ترغب في اقتناءه.
Mwingi wa kukodolea macho : Huyo ni yule (mwanamke) ambaye hutupia jicho lake kila kitu na hupenda kukimiliki.
🟪 براقة: هي التي تشتغل بنفسها عن بيتها و زوجها ما يعرف (بالأنانية).
Mwenye kujing’arisha mno : Huyo ni yule (mwanamke) ambaye hushughulika na nafsi yake na akaiacha nyumba yake na mumewe ni ile (tabia) inayojulikana kwa (ubinafsi).
🟫شداقة: تتشدق بالكلام ، اي كثيرة الكلام و قليلة السكوت.
Mwingi wa kubwabwaja :
Hukunjua kinywa chake kwa kuzungumza, maana yake : Ni mwingi wa kuzungumza na mchache wa kunyamaza.
💠 الشيخ سليمان الرحيلي حفظه الله.
Maelezo ya mfasiri :
Hawa ni wanawake wa sampuli tano ambao mwanamume anatakiwa achukue tahadhari nao asije akawaoa ,na kwa ufafanuzi zaidi ili wafahamike :
1- Wa kwanza ni mwanamke ambaye hukithirisha kuugulia na kulalamika yaani kila siku ni kumlalamikia mumewe mara hili mara lile, na kila anachofanyiwa haridhii na kile anachopewa hakipendi, na haishi maisha ya raha na mumewe kwa sababu ya kumsumbua kwake mumewe na bila shaka mwanamume mwenye kuishi na mwanamke huyu hatopata raha katika maisha.
2- Wapili ni mwanamke mwenye kuwa na shauku na hamu ya kuolewa na mwanamume mwengine na hali yupo katika ndoa na kwa kulidhihirisha kwake hilo mwanamke huyo hujiona kuwa yeye ni mbora zaidi ya mumewe na wala hakustahiki kuolewa na yeye !.
3- Watatu ni yule mwanamke mwenye kutizama kila kitu na kukipenda kila kitu akionacho ,mfano :Akiona nguo anaitaka, akiona kiatu anakitaka, akiona chakula kizuri anakitaka!
4- Wanne ni yule mwanamke anayeishughulikia nafsi yake kwa kujipamba na kujiremba na kwa mambo mbalimbali na haishughulikii familia yake na hata mumewe kwa kifupi huyu ni mwanamke mbinafsi ambaye anaijali nafsi yake tu!
5- Watano ni mwanamke ambaye mwingi wa kuzungumza na kubwabwaja muda mwingi huzungumza tu na kunyamaza kwake ni nadra au tunaweza kusema kuwa mdomo wake ni kama kinanda!
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 13, 1443H ≈ Aug 11 15, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•