🔸 قال الشيخ/ ابن عثيمين رحمه الله:
Amesema sheikh
فالذين يبيعون على الناس بالغش – ولا سيما أهل الخضار – فإن كل مالٍ، بل كل قرش يدخل عليهم من زيادة في الثمن بسبب الغش فإنه حرام،
Basi wale ambao wanawauzia watu kwa hadaa na haswa wauza mboga mboga na bila shaka kila mali bali kila senti inayoingia kwao inayotokana na kuzidi thamani (ya bidhaa) kwa sababu ya hadaa basi (hilo chumo) ni haramu,
فالذين يغشّون في البيع أو في الشراء يرتكبون محظورين:
Basi wale ambao wanafanya hadaa katika kuuza au katika kununua (watu hawa) hufanya madhambi mawili:
المحظور الأول: العدوان على إخوانهم المسلمين بأخذ أموالهم بغير حق.
Dhambi ya kwanza : Kuchupa mipaka /kuwafanyia uadui ndugu zao waislamu kwa kuchukua mali zao bila ya haki .
والمحظور الثاني: أنهم ينالون تبرّؤ النبي ﷺ منهم، وبئس البضاعة بضاعة يلتحق فيها صاحبها بالبراءة من رسول الله ﷺ.
Na dhambi ya pili: Kwamba wao wanapatwa na (dhambi) ya kujiepusha nao Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie- na bidhaa mbaya kabisa ni bidhaa (ambayo) mwenye (bidhaa) hiyo anakutana na (dhambi) ya kujiepusha na Mtume wa Allah – swala na salamu za Allah zimfikie-
📚 انظر: شرح حديث رقم (١١١) من رياض الصالحين
Maelezo ya mfasiri:
Mwenye kufanya hadaa katika biashara anakuwa imefanya madhambi ya aina mbili:
1- Kuchupa mipaka na kuwafanyia uadui ndugu zake waislamu , na Allah -aliyetukuka- amekataza kuwafanyia uadui/Kuchupa mipaka katika aya nyingi , amesema mwanachuoni mkubwa Assa’diy -Allah amrahamu-:
والله قد نهى عن الاعتداء فقال :
Na Allah bila shaka amekataza kuchupa mipaka /kufanya uadui akasema:
{ وَلَا تَعْتَدُوٓاْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلْمُعْتَدِينَ }
{Na wala musichupe mipaka bila shaka Allah hawapendi wenye Kuchupa mipaka}
البقرة ١٩٠
Kisha akasema Assa’adiy- Allah amrahamu-:
بل يبغضهم ويمقتهم ويعاقبهم على ذلك .
Bali (Allah) anawachukia na anawachukia mno na atawaadhibu juu ya hilo .
تفسير السعدي
Na katika hadithi kumekuja hadithi nyingi zinazokemea kuchupa mipaka juu ya haki za watu na kuwafanyia uadui miongoni mwa hizo ni kauli yake Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-:
«المُسْتَبَّانِ ما قالا فَعَلى البَادِي منهما مَا لَمْ يَعْتَدِ المَظْلُوم».
Watukananao wawili (matusi yote) waliyoysema (dhambi) ni ya yule aliyeanza (kutukana) katika wao maadamu hakuchupa mipaka (yule) aliyedhulumiwa.
رواه مسلم
Maana ya hadithi:
Watu wawili wenye kutukanana mwenye kupata madhambi ni yule aliyeanza kumtukana mwenzake ,ama huyu aliyeanza kutukanwa yeye hana madhambi kwa sababu ameruhusiwa kumrudishia yule anayemtukana ila akichupa mipaka kwa kumrudishia matusi zaidi hapo atapata madhambi zaidi ya yule aliyeanza kumtukana.
2- Dhambi ya pili ni dhambi ya kuwa mbali na Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie- ,na ukiona yoyote ambayo Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- amejitenga na kujiweka mbali na mwenye kufanya dhambi hiyo basi tambua kuwa hiyo ni dhambi kubwa ,kama vile dhambi hii ya kufanya hadaa ,kwa sababu Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- amesema:
{ مَنْ غَشَّ فَليس مني }
Mwenye kufanya hadaa basi (huyo) si katika mimi}
رواه مسلم.
Maana yake : Kufanya hadaa hayupo katika njia yangu na mwenendo wangu kwa maana amefanya dhambi kubwa.
Mwisho:
Kama alivyosema sheikh kuwa wenye kufanya biashara kwa hadaa kwa sana wauza mboga mboga :Kama vile nyanya au bamia huwenda wakamuwekea mtu bamia zilizokomaa tupu !
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 20, 1443H ≈ Jan 22, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•