Tahadharini na uhizbiyyah (ukikundi) na tahadharini na makundi

https://t.me/fawaidussalafiyatz

احذروا الحزبية احذروا الجماعات!

TAHADHARINI NA UHIZBIYYAH (UKIKUNDI) NA TAHADHARINI NA MAKUNDI!

قال العلامة ابن عثيمين – رحمه الله تعالى- :

Amesema mwanachuoni mkubwa ibn ‘Uthaimin – Allah amrahamu-:

يجب على طالب العلم أن يتخلى عن الطائفية والحزبية، بحيث يعقد الولاء والبراء على طائفة معينة، أو على حزب معين, السلف الصالح ليسوا أحزابا، بل هم حزب واحد، ينضوون تحت قول الله عز وجل: { هو سماكم المسلمين من قبل } فلا حزبية، ولا تعدد، ولا موالاة، ولا معاداة، إلا على حسب ما جاء في الكتاب والسنة.

Inawajibika kwa mwanafunzi ajiepushe na ukikundi na ukikosi kwa upande ambao (akawa) anayafunga mapenzi na kuchukia kwa kundi maalumu au kikosi maalumu, wema waliopita hawapo vikundi vikundi, bali wao ni kikundi kimoja, (wote) wanashirikiana chini ya kauli yake Allah – aliyeshinda na kutukuka – :

{ Yeye amewaita waislamu kabla }

Basi hakuna ukikundi na wala hakuna kukithiri makundi na wala hakuna kupendana na wala kuchukiana ila kwa kadri ya vile ilivyokuja katika qurani na sunnah.

المصدر: كتاب العلم، الصفحة (٦٠/ ٦١)

Maelezo:

Daawatu ssalafiyyah yaani ulinganiaji unaofuata mfumo wa wema waliopita, kwa maana uislamu halisi; Watu hawa hawana sifa ya kujiwekea kikundi wakawa kila anayeendana na wao basi ni mwenzao, kila anayetokea nchi yao ni mwenzao, kila anayetokea mkoa wao ni mwenzao, kila anayetokea katika maeneo yao ni mwenzao! Na ikawa ambae hatokei eneo lao au mkoa wao wanambagua! Mwenye tabia hii ajue kuwa amejiwekea kikundi hata kama unadai kuwa wewe ni salafi. Ukabila na chuki za kubagua watu kwa sababu hawapo na watu fulani huu ni uhizbiayyah wa wazi na hili ni gonjwa linalotafuna safu za waislamu na masalafi haswa. Usalafi ni dini na yeyote atakayesimama sawa sawa katika dini yaani suna akashika sawa sawa mwenendo wa wema huyo ni salafi hata kama hatokei mkoa wako au hamjui Sheikh wako. Tanbihi: Mizani ya kupendana na kuchukiana ni lazima ipimwe na qura’ni na suna na wala si kwa matamanio ya nafsi.

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Tembelea website yetu: ☟ https://www.fawaidusalafiya.net Telegram bonyeza hapa: ☟ https://t.me/fawaidussalafiyatz 🗓️ Imechapishwa: Rajab 11, 1442H ≈ February 23, 2021M,

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾 https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *