TATIZO NYOYO ZETU HAZIJASALIMIKA!

‏عن سفيان بن دينار – رحمه الله- قال:

Kutoka kwa Sufiani bin Dinar – Allah amrahamu – Amesema :

«قلت لأبي بشير وكان من أصحاب علي بن أبي طالب رضي الله عنه:

Nilimwambia Abuu Bashir na (huyu) alikuwa ni katika watu wa Aliy bin Abii Twalib-Allah amridhie – :

أخبرني عن أعمال من كان قبلنا،

(Hebu) nielezee kuhusu ibada za wale waliopita kabla yetu (maswahaba)

قال: كانوا يعملون يسيراً ويؤجرون كثيراً،

Akajibu : Walikuwa wakifanya (matendo) kwa uchache na na wakilipwa (thawabu) kwa wingi,

قال: ولم ذاك؟ قال: لسلامة صدورهم»

akauliza (tena) : Ni kwa sababu gani (imekuwa) hivyo?

Akajibu : Kwa sababu ya usalama wa vifua vyao.

  • الزهد لِهَنَّادِ بْنِ السَّرِي | ٢/٦٠٠

Maelezo ya mfasiri :

Moyo safi usiokuwa na husuda wala mafundo na chuki, ni katika sifa za nyoyo za watu wema waliopita, na hapa watu wa kwanza kabisa wanaokusudiwa ni maswahaba na wale waliowafuata kwa wema baada yao, na hii ndiyo sababu ya wao kuwa walikuwa wakifanya matendo machache na wakilipwa thawabu nyingi, na bila shaka mwenye moyo safi uliosalimika na maradhi hayo tuliyoyataja hapo juu mtu huyu huwa na ikhlaswi kwa maana hufanya matendo yake kwa ajili ya Allah, ama mwenye husuda na mafundo ya moyo hii ni dalili ya kukosa ikhlaswi.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 1, 1445H ≈ Nov 15, 2023M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *