◾️يقول السائل :
Anasema muulizaji :
ما العلاج المناسب لانشراح الصدر ، حيث إنني أعيش في ضيق شديد ، أفتوني مأجورين
Ni ipi tiba sahihi ya kukikunjua kifua, kwani mimi naishi katika dhiki kubwa, nipeni fatwa hali (nyinyi) ni wenye kulipwa (kwa majibu yenu).
الجواب :
Jawabu :
« العلاج المناسب هو كثرة ذكر الله – عز وجل – قال الله تعالى
Tiba sahihi ni kukithirisha kumtaja Allah – aliyeshinda na kutukuka -amesema Allah – aliyetukuka – :
{ ۗ أَلَا بِذِكْرِ اللَّهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ}
{ Sikilizeni kwa kumtaja Allah nyoyo hutulizana}
☜ ومن العلاج ألا يهتم الإنسان بأمور الدنيا ، وألا يكون له هم إلا الآخرة .
Na miongoni mwa tiba ni mtu kutotilia umuhimu mambo ya dunia, na asiwe na makusudio (moyoni mwake) isipokuwa akhera.
☜ ومن العلاج أن يكون الإنسان باذلا لمعروفه ،
Na katika tiba ni mtu kuwa ni mwenye kutoa mazuri yake,
سواء ببذل المال ، أو ببذل المنافع ،
sawa sawa kwa kutoa mali, au kutoa manufaa (mbalimbali)
وبذل البدن يساعد إخوانه ،
na kutoa nguvu zake kwa kuwasaidia ndugu zake (waislamu)
أو ببذل الجاه ، فإن هذا يوجب انشراح الصدر .
au kukitoa cheo chake (kwa kutoa msaada), basi bila shaka (kufanya) haya husababisha ukunjufu wa kifua.
☜ وليكثر أيضا من هذا الدعاء :
” رَبِّ اشْرَحْ لِي صَدْرِي وَيَسِّرْ لِي أَمْرِي“
Na akithirishe pia dua hii:
“Ewe Mola wangu mlezi! Nikunjulie kifua changu. Na unifanyie wepesi mambo yangu
📚 فتاوى نور على الدرب لابن عثيمين (١٢/٢٢).
Maelezo ya mfasiri :
Hizi ni tiba za kuondoa dhika na tabu anayoihisi mtu moyoni mwake :
1- Kukithirisha kumtaja Allah, kwa sababu kumtaja Allah huleta utulivu katika nafsi ya muumini raha ambayo hata wafalme na matajiri hawaipati, na ndiyo maana wapo waliofikia kusema katika wema waliopita baada ya kuhisi ile raha na utulivu waliokuwa nao katika nafsi zao :
“لو يعلم الملوك وأبناء الملوك ما نحن فيه من النعيم لجالدونا عليه بالسيوف”
“Lau wangejua wafalme na watoto wa wafalme ile (hali) ya neema tuliyokuwa nayo (basi) wangetupiga mapanga”.
2- Tiba ya pili ni kuipuuza dunia na kutoiweka mbele na kutoyakodolea macho mapambo yake, lna ndiyo maana wanasema wanawachuoni kuwa unapokiona kitu na ukapendezewa nacho useme hivi :
لبيكَ ، إنَّ العيشَ عيشُ الآخرة
(Mimi) ni mwenye kulazimiana na twaa yako, bila shaka maisha hasa ni maisha ya akhera.
3- Kufanya mema na kheri mbalimbali ni sababu ya kupata ukunjufu wa moyo kwa sababu yule mwenye kufanya mema mbalimbali kama vile kutoa sadaka, na kuwasaidia watu kwa nguvu zake na cheo chake, na akafanya hivi kwa kutaraji malipo kutoka kwa Allah bila shaka muislamu huyu hupata utulivu na ukunjufu wa kifua kwa sababu anajua kuwa haya matendo anayoyafanya atakuja kulipwa
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 5, 1445H ≈ Nov 19, 2023M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•