Tiba ya uvivu katika kutafuta elimu ya kisheria.

Allah awalipe kheri; Sheikh Swaalih: Uvivu ambao humtokea mwenye kutafuta elimu katika kutafuta kwake elimu na kuchukua masurufu katika elimu ya kisheria, ni ipi tiba yake ewe sheikh?

(Jawabu):

Kwa ajili hiyo tumesema: Hakuna budi (kuwa na) subira,

(Mtangazaji): Ndio ewe Sheikh,

(Sheikh); Na yule ambaye hakuonja udhalili wa kujifundisha punde atakunywa kinywaji cha ujinga maisha yake yote, kama anavyosema imamu Shafii – Allah amrahamu – basi hakuna budi kusuburi juu ya mashaka ya kutafuta elimu, hakuna budi kuvumilia na hakuna budi urefu wa muda (muda urefuke). Na elimu haina mwisho, lakini uchukue katika kila kauli ile iliyokuwa nzuri zaidi. ” Hakika si vinginevyo elimu ni kama bahari yenye maji mengi, basi chukua katika kila kauli ile iliyokuwa nzuri zaidi ” Kusubiri, hakuna budi kusubiri, hakuna budi kuwa na nia njema. Akiwa mtu ana nia njema humsukuma kuelekea kutafuta elimu (ya kisheria/dini). Na pindi atakapoonja ladha (utamu) wa elimu, basi bila shaka huyo (mtu atakuwa) anajisikia raha kwa hiyo (elimu) na anasahu tabu /uchovu. Pindi atakapoonja utamu wake na ladha yake (husahau tabu). Ndio

Mjibuji Swali: Sheikh Swaalih Fauzaan Al-fauzaan

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Kiunganishi cha sauti ya Sheikh: https://youtu.be/SmWVw9hr4gc

Imeandaliwa: Tarehe 04 – Safar – 1442H ≈ 21 – September – 2020M.

Kupata faida nyingi tembelea website yetu kwa kubonyeza hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

Usikose kuungana nasi Telegram kwa kubonyeza hapa: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Muhimu: Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *