TOFAUTI YA KUKUTANA NA UOVU KATIKA MAZISHI NA UOVU KATIKA HARUSI !

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

TOFAUTI YA KIFIQIH !

PINDI UNAPOKUTANA NA UOVU KTK MAZISHI NA UNAPOKUTANA NA UOVU KTK HARUSI !

لماذا لا يرجع إذا رأى منكرا في الجنازة و يرجع في منكر العرس ؟

Kwanini (mtu) harudi (haondoki) pindi atapoona uovu katika jeneza (mazishi) ,na (anatakiwa) arudi (atapoona) uovu katika harusi ?

قــال العلامة ابن القيم رحمه الله:

Amesema mwanachuoni mkubwa ibn l-Qayyim- Allah amrahamu-:

▫️ «وقد نص الإمام أحمد على أن الرجل إذا شهدالجنازة فرأى فيها منكراً لا يقدر على إزالته أنه لا يرجع، ونص على أنه إذا دُعي إلى وليمة عرس فرأى فيها منكرا لايقدر على إزالته أنه يرجع ‏،فسألت شيخنا عن الفرق ؟

Na bila shaka ametaja imamu Ahmad kuwa pindi mtu anapohudhuria jeneza (mazishi) ndani yake kukawa na uovu (na yeye) hawezi kuuondoa ,(anatakiwa) asirudi, na akataja (tena kuwa) kuwa huyo (mtu) akiitwa katika karamu ya harusi na akaona ndani yake uovu asioweza kuuondosha (anatakiwa) arejee.

Basi nikamuuliza shekhe wetu (ibn Taimiyyah) kuhusu tofauti (hii)?

⏪ فقال: لأن الحق في الجنازة للميت، فلا يُترك حقُّه لما فعله الحيّ من المنكر، والحق في الوليمة لصاحب البيت، فإذا أتي فيها بالمنكر، فقد أسقط حقه من الإجابة.

Basi (ibn Taimiyyah) akajibu :

Kwa sababu haki katika jeneza (mazishi) ni ya maiti ,basi haiachwi haki yake kwa sababu ya aliyoyafanya aliyekuwa hai katika maovu ,na haki katika karamu ya harusi ni ya mwenye nyumba ,basi akileta ndani yake uovu bila shaka imeidondosha haki yake ya kujibu (huo wito).

📚 إعلام الموقعين (١٢٠/٦).

Maelezo ya muandaaji :

Ufupi wa maana ya maneno haya ni huu :

Imamu Ahmad- Allah amrahamu- ameeleza kuwa mtu anapohudhuria mazishi ya ndugu yake muislamu na akaona uovu ndani yake anatakiwa asiondoke ,ama akiitwa katika karamu ya harusi na akakuta kuna uovu ndani yake na akawa hana uwezo wa kuuondoa basi ni wajibu aondoke ,na kama anaweza kuundoa kama vile akawa ni mtu mwenye mamlaka basi auondoe huo uovu.

Ibn l-Qayyim -Allah amrahamu- akamuuliza sheikhe wake kuhusu hii tofauti ,akamjibu :

Haki ya kuhudhuria jeneza na mazishi ni ya huyu muislamu aliyekufa kwa hiyo hauwezi kuiacha haki yake kwa uovu uliofanywa na yule aliyekuwa hai, kama alivyoeleza Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- pindi alipotaja haki za muislamu juu ya muislamu sita au tano ,na akataja katika hizo :

واتباع الجنائز

Kusindikiza majeneza (kuzika) .

Kwa maana hii ni haki ya maiti .

Ama kuhudhuria karamu ya harusi ni haki ya huyo mwenye harusi kama alivyoeleza Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie- katika hizo haki sita za muislamu :

وإجابة الدعوة،

Na kujibu wito (wake) .

Na katika riwaya nyingine:

وإذا دعاك فأجبه

Na pindi (muislamu) atapokuita basi mjibu .

Hadithi hii kwa riwaya zake zote mbili inajulisha kuwa ni wajibu kwa muislamu kujibu wito wa muislamu na makusudio ya wito ni kuhudhuria karamu ya harusi kama walivyoeleza wanachuoni wengi zaidi ,na kujibu huu wito ni haki ya yule mwenye hiyo karamu ya harusi kwa hiyo kama kuna uovu ndani yake ule uwajibu wa kuhudhuria unadondoka tena ni haramu kuhudhuria ila yule mwenye uwezo wa kuuondosha huo uovu .

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qa’adah 4, 1442H ≈ June 14, 2021M.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *