TUJIKUMBUSHE KATIKA KUWAFAHAMU MASHIA (15) .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

​من كفريات الخميني-الهالك-​

MIONGONI MWA (MANENO YA) KIKAFIRI YA AL-KHOMAINIY (MWENYE KUANGAMIA)​

​صحائف الأعمال تعرض على مهدي الرافضة​

SAHIFA /MADAFTARI YA MATENDO YANADHIHIRISHWA JUU YA MAHDIY WA MASHIA!!

قال الخميني -الهالك:-

AMESEMA AL-KHOMAINIY- MWENYE KUANGAMIA:-

” إن صحائف أعمالنا تعرض على الإمام صاحب الزمان (سلام الله عليه) مرتين في الأسبوع حسب الرواية “

HAKIKA SAHIFA ZA MATENDO YETU HUDHIHIRISHWA JUU YA IMAMU ​MWENYE ZAMA/AL-MAHD (AMANI YA ALLAH IWE JUU YAKE) MARA MBILI KWA WIKI KWA KADRI YA (VILE) RIWAYA (ZILIVYOKUJA)

📚 REJEA:

​انظر كتاب “المعاد في نظر الإمام الخميني ” ص ٣٦٨​
[ Angalia kitabu ” Al-ma’ad fii nadhwar Al-imam Al-khomainiy” ukurasa wa 363 ]

MAELEZO YA MWANDISHI: ✍🏾

​Hadithi zilizothibiti zinaeleza kuwa matendo hunyanyuliwa kwa kupelekwa kwa Allah kila juma tatu na al-khamisi kwa wiki, na usiku na nchana kila siku.

Na pia hunyanyuliwa katika nusu ya mwezi wa Sha’aban kwa mwaka mara moja katika hadithi ambayo wameisahihisha baadhi ya wanachuoni na hili lakupandishwa matendo kwa Allah hufanywa na malaika kwa hekima maalumu ambayo yeye mwenye Allah anaijua pamoja na kuwa Allah anajua kila kitu na hakuna jambo linalompita.

Lakini Mshia huyu anasema kuwa matendo yaliyoandikwa katika sahifa /madaftari hudhihirishiwa Imamu wao wa kubuni ambaye yupo pangoni ambaye anasubiriwa kutoka!, na cha ajabu haifahamiki atatoka lini! lakini kubwa zaidi ni kwamba yeye huyo imamu wamempa nafasi ya Allah ya kudhihirishiwa matendo ya wanadamu yaliyoandikwa katika madaftar ambayo huifadhiwa na malaika!!​

Na huyu Khomainiy ndiye imamu wa Mashia katika zama hizi na ndiye marejeo yao ! je ikiwa imamu wao anaitikadi hizi za kikafiri je wafuasi wake watakuwa vipi ?!

━════════ ۞
Mwandishi: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

════════━
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️Iliandaliwa November 23,2017M, Tolea la pili: Swafar/Mfungo tano 21, 1443H ≈ September 28, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *