TUJIKUMBUSHE KATIKA KUWAFAHAMU MASHIA .
Makala namba (4) :
هذا هو الخميني لمن لا يعرفه!
HUYU NDIYE KHOMEINY KWA WALE WASIO MJUA!
Khomainy ni mwanachuoni mkubwa wa Mashia katika zama hizi hebu mwangalie Omar Mayunga pindi alipokuwa anunukuu maneno kutoka kwa imamu wake huyu kama wanavyomuita:
” …Ndipo Muasisi wa mapinduzi ya Serikali ya Kiislamu ya Iran,Imam Ruhullah Al-Musawy Al-khomainy…”
📚 Rejea:⇊
[ Angalia Qur’an inayobainisha Tarjama na Tafsiri Kiarabu na Kiswahili,ya Aliy Juma Mayunga,ukurasa wa 518 ]
✍🏾 Baada ya kujua uzito wa MTU huyu kwa Mashia hebu sasa angalia itikadi aliyokuwa nayo ambayo ni ya ukafiri kabisa:
قال الخميني- :-
Amesema Khomainy -:
“لنا مع الله حالات هو نحن ، ونحن هو، وهو هو، ونحن نحن “
“Sisi (Maimamu) tuna hali (mbalimbali) pamoja na Allah (muda nwingine) Yeye (Allah) ndiye sisi na sisi (ndiye) Allah na yeye (Allah ) ni yeye na sisi ni sisi “
📚 Rejea:⇊
شرح دعاء السحر ١٠٣
[ Sherh Du’aau ssahr 103 ]
✍🏾 MAELEZO YA MWANDISHI:-
Maana ya maneno haya ni kuwa Khomainy anaitikadi ya wahdat lwujuud yaani itikadi ya kuamini kuwa kila unachokiona ni Allah!
Ni ile itikadi Ibn ‘Arabiy na wengineo ambao wanachuoni wamewakufurisha lakini kwa masikitiko makubwa kuwa mtu huyu katika dini ya kishia ni MTU mzito mno tena ni Imamu!
Kama alivyomuita Mayunga, na Mashia wenzake na mimi nakumbuka katika miaka ya nyuma kulikuwa na jarida likiitwa sauti ya umma lililokuwa likiandikwa kwa lugha ya Kiswahili jarida hill liliupamba na kuuneza sana ushia pamoja na kumpamba Khomainy na serikali Yake ya Kishia!
basi tambua kuwa hii ni miongoni mwa itikadi za huyu Khomaini yaani kuna muda yeye anakuwa Allah! na Allah anakuwa yeye! .
Ametakasika Allah na uchafu huu utakasifu mkubwa-.
✍🏾
Mwandishi: Ismail Seiph Mbonde .
━════════ ۞ ════════━
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Toleo la kwanza: Mfungo tano 19,1439 H ,sawa na tar.8/11/2017 M, Toleo la pili : Mfungo tatu 29, 1442H ≈ August 8, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•