قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
Amesema mjumbe wa Allah – swala na salamu za Allah ziwe juu yake:
” لا تصوموا هذه الأيام، فإنها أيام أكل وشرب وذكر لله عز وجل “
” Msifunge masiku haya, bila shaka masiku hayo ni masiku ya kula na kunywa na kumtaja Allah – aliyeshinda na aliyetukuka “
📚 رواه أحمد (10286) وصححه الألباني في السلسلة الصحيحة (3573).
قال ابن رجب الحنبلي – رحمه الله:
Amesema Ibn Rajab Al-Hanbaliy – Allah amrahamu –
فأيام التشريق يجتمع فيها للمؤمنين نعيم أبدانهم،
Basi masiku ya kukausha (nyama) kunakusanyika ndani yake kwa waumini neema za viwiliwili vyao,
بالأكل والشرب ونعيم قلوبهم بالذكر والشكر.
Kwa kula na kunywa na neema za nyoyo zao kwa kumtaja Allah na kumshukuru.
📚لطائف المعارف (٢٩١/١)
قال النووي – رحمه الله
Amesema Annawawiy – Allah amrahamu –
ويستحب الإكثار في أيام التشريق من الأذكار،
Inapendeza kukithirisha katika masiku (haya) ya tashriq kukithirisha nyiradi,
وأفضلها قراءة القرآن.
Na bora yake ni kusoma Qur’ani.
📚 الأذكار (٣٣٩)
Maelezo kutoka kwa mfasiri – Allah amuhifadhi
Masiku ya kusambaza nyama na kuzikausha (tashriq) nazo ni siku tatu zinazofuata baada ya sikukuu ya kuchinja yaani tarehe 11,12,13 .
Hizi ni siku ambazo kuna neema kubwa kwa waislamu, ni siku za watu kula na kunywa kwa maana ni masiku ya kuneemeka viwiliwili na miili ya waislamu na ni siku za kumtaja Allah.
Na ni haramu kufunga masiku haya funga yoyote na hii ndiyo kauli mpya ya imamu Shafi-Allah amrahamu- ambayo inayotegemewa katika madhehebu yetu ya kishafii hata kwa haji mutamatti’i aliyekosa mnyama wa kuchinja pia haruhusiwi kufunga , lakini madhehebu ya Ahmad wao wanaona kuwa mutamatti’i anaruhusiwa kufunga na madhehebu ameyapa nguvu Nawawiy katika majumu’u .
Tanbihi: Yameitwa masiku ya kukausha nyama kwa sababu zamani walikuwa wakizisambaza nyama na kuzikausha juani katika masiku haya ama katika zama hizi Allah -aliyetukuka- ametupa neema ya mafriza ,lakini ubora wa haya masiku na ibada zilizomo ndani yake zinabakia vile vile .
الله أكبر الله أكبر لا إله إلا الله والله أكبر، الله أكبر ولله الحمد.
Takbirah hizi mwisho wake ni baada ya swala ya alasir tarehe 13 .
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tatu 11, 1445H ≈ Jun /17, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•