كتب الشيخ صالح العصيمي -حفظه الله تعالى- عبر حسابه على تويتر .
Ameandika sheikh Swaleh Al-Uswaim -Allah amuhifadhi- kupitia ukurasa wake wa twitter (maneno yafuatayo) :
زهرة العمر لا تذبل حين تصير ثمرةً يُنتفع بها في الدُّنيا والآخرة،
Ua la umri halitonyauka pindi litapokuwa (ua hilo) ni tunda lenye manufaa dunia na akhera
فاغتنموا قوَّتكم قبل ضعفكم، وصحَّتكم قبل مرضكم،
Basi tumieni fursa ya nguvu zenu kabla ya udhaifu wenu ,na afya zenu kabla ya maradhi yenu ,
واسقوا شجرة أعماركم لتزهر ثمَّ تثمر: علمًا نافعًا أو ولدًا صالحًا أو صدقةً جاريةً.
Na imwagilieni miti ya matendo yenu ili itoe
maua kisha itoe matunda : (ambayo ni) elimu yenye manufaa au mtoto mwema au sadaka yenye kuendelea .
Maelezo ya mfasiri:
Maisha ya dunia ni kama mti /mmea uliotoa maua kama utaumwagiliwa vizuri basi utatoa matunda ambayo watu watanufaika nayo na huu ndiyo mfano wa mtu mwenye kufanya matendo mema kwani matendo hayo yatamnufaisha duniani na akhera kisha sheikh -Allah amuhifadhi- akahimiza kutumia nguvu zetu kabla ya kufikiwa na hali ya udhaifu muda ambao mtu hatoweza kujipinda katika ibada ,na pia akahimiza kukitumia kipindi cha afya kabla ya kufikwa na maradhi ,na akahimiza kukithirisha kufanya mema na hasa yale matendo ambayo ujira wake haukatiki kama alivyosema Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie- :
((إذا مات الإنسانُ انقطع عنه عملهُ إلا من ثلاثةٍ:
Anapofariki mwanadamu humkatikia matendo yake ila yanayotokana na (mambo) matatu :
إلا من صدقة جارية، أو علم ينتفع به، أو ولد صالح يدعو له))؛
ila (thawabu) zinazotokana na sadaka yenye kuendelea,au elimu yenye manufaa, au mtoto mwema mwenye kumuombea dua (mzazi)”
رواه مسلم
Ufafanuzi :
Haya ni mambo matatu ambayo mtu anapoyaacha baada ya kufa basi thawabu zake humfikia :
1-Sadaka yenye kuendelea,kama vile akachimba kisima, akajenga madrasa n.k
2- Elimu yenye manufaa ,mfano yule aliyesoma elimu ya kisheria kisha akaifundisha au akatunga vitabu basi thawabu za manufaa ya elimu hiyo zitaendelea kumfikia .
3- Mtoto mwema :
Amesema sheikh Al-albaaniy – Allah amrahamu:
ما يفعله الولد الصّالح من الأعمال الصّالحة، فإنّ لوالديه مثل أجره، دون أن ينقص من أجره شيء،
Yale anayoyafanya mtoto mwema katika matendo mema basi bila shaka wazazi wake wawili wanapata mfano wa ujira anaopata bila ya kupungukiwa (huyo mtoto) chochote (katika) ujira wake,
لأنّ الولد من سعيهما وكسبهما وقد قال – ﷺ –
Kwa sababu mtoto ni katika juhudi zao hao (wazazi) na chumo lao na bila shaka amesema (Mtume) – swala na salamu za Allah zimfikie –
إنّ أطيب ما أكل الرجل من كسبه، وإنّ ولده من كسبه.
Bila shaka kizuri zaidi alichokula mtu ni kile kinachotokana na chumo lake na bila shaka mtoto wake ni katika chumo lake.
📚 المصدر: أحكام الجنائز ١٢٦/١)
Maana ya maneno ya sheikh :
Hadithi hii ni dalili ya kuwa kila analolifanya mtoto katika matendo mema basi mzazi ananufaika kwa thawabu hizo lakini kwa sharti ikiwa mzazi huyo alikuwa ni sababu ya kufanywa mema hayo,kama vile akamlea mwanae katika dini na kumpa muongozo katika mema,
Bila shaka mzazi atanufaika na mema ya mtoto wake, na kinyume chake ikiwa mzazi ni kikwazo na ni kuzuizi kwa mwanae katika kufanya kheri basi mzazi huyo badala ya kupata thawabu atapata dhambi ya kuwazuia watu katika kheri!
Na hapa tunawazindua wazazi ambao wamekuwa ni vikwanzo kwa watoto wao pindi wanapotaka kuisoma dini ya Allah tena ni elimu ya wajibu kwao!
Tanbih:
Ama hadithi tuliyoitaja hapo juu inayozungumzia kuwa mwanadamu muislamu pindi anapofariki matendo yote hukatika kwake ila vitu kadhaa vilivyotajwa katika hivyo;
” أو ولد صالح يدعو له “
“ Au mtoto mwema anayemuombea dua ”
Hadithi hii haina maana kuwa mzazi hanufaiki na matendo ya mwanae mpaka mtoto amuombee dua mzazi wake, bali makusudio ya maneno haya ya Mtume ni kumuhimiza huyu mtoto juu ya kumuombea dua mzazi wake yaani baba yake au mama yake,
Ama thawabu humfikia mzazi hata kama mtoto hajakusudia mfano wake ni kama mtu aliyepanda mti watu wakawa wanakula matunda ya mti huo basi thawabu hupata yule aliyeupanda ule mti sawa sawa yule aliyekula lile tunda akimuombea aliyeupanda mti au hajamuombea,
Au maana ya pili ya hadithi hii ni kuwa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – amesema hivi kwa kubainisha hali ilivyo yaani anakusudia kuwa mtoto mwema ndiye anayemkumbuka mzazi wake.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 26, 1444H ≈ Oct 22, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•