كتب الشيخ صالح العصيمي -حفظه الله تعالى- عبر حسابه على تويتر .
Ameandika sheikh Swaleh Al-Uswaim -Allah amuhifadhi- kupitia ukurasa wake wa twitter (maneno yafuatayo) :
من شرار الخلق قومٌ يتَّخذون الدِّينَ مطيَّةً يتوصلون بها إلى الدُّنيا، فتراهم يركضون وراء المال والرِّئاسة والجاه،
Miongoni mwa viumbe waovu zaidi ni watu wanaoifanya dini kuwa ni kipandwa wakaifanya kuwa ni njia ya kuipatia dunia basi utawaona wanaenda mbio nyuma ya (kutafuta) mali na uongozi na vyeo,
ويظلمون غيرهم في سبيلها، ولا يأبون قلب الشَّكل لأجل الأكل.
na (utawaona) wakiwadhulumu wengine katika njia ya (kuitafuta) hiyo (dunia) na wala hawajali kupindua uhalisia wa mambo kwa ajili ya kula .
الاثنين ٢٢ صفر ١٤٤٤ه
Maelezo ya mfasiri :
Miongoni mwa watu wabaya ni hawa wenye kuitafuta dunia kupitia dini na utawakuta wakitafuta mali,uongozi,vyeo tena wapo tayari kubadilisha uhalisia wa mambo,
kama vile kuwaponda wengine, kuleta fitna , na hii ni alama ya kukosa ikhlaswi na kuitafuta dunia kupitia dini ni miongoni mwa mambo ambayo yalielezwa kuwa yatakuja kutokea ,kama ilivyothibiti kutoka kwa Omary bin Al-khattwab -Allah amridhie- siku moja alipanda juu ya membari akawahutubia waislamu na akataja fitna na mabalaa mbalimbali yatakayotokea baadae ,na Aliy bin Abii Twalib -Allah amridhie-alimuuliza Omary ,Ni muda gani yatatokea hayo mabalaa ?, kisha Aliy akalijibu swali hilo mwenyewe akasema :
” إذا تـُفُـقِّـهَ لغير الدِّين، وتـُعُلِّمَ لغيرِ العَمَلِ، والتُمسَتِ الدنيا بعملِ الآخرة“
“ Pindi kutakapotafutwa elimu ya dini si kwa ajili ya dini, na kukatafutwa elimu bila ya kuifanyia kazi , na kukatafutwa dunia kwa matendo ya akhera ”
المصنف لعبد الرازق الصنعاني ( ج ١١ ص٣٦٠)
Ufafanuzi :
Maana ya athari hii ni kuwa hayo mabalaa yatatokea pindi watu watapokuwa wanaisoma dini ya Allah lakini si kwa ajili ya dini bali ni kwa malengo yao mengine, na watu wakaisoma dini ya Allah bila ya kuifanyia kazi ,na watu wakawa wanaitafuta dunia kwa kutumia matendo ya kuitafuta akhera ambayo ni ibada.
Tanbih :
Maneno kama haya yanayohusu mambo ya ghaibu kama haya aliyoyazungumza Aliy -Allah amridhie- yanapewa hukumu ya maneno ya Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-kwa sababu swahaba hawezi kuongea habari hizi kwa akili yake kama walivyoeleza wanawavyuoni .
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 1, 1444H ≈ Oct 26, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•