UBAYA WA KUMDHALILISHA MKE

‏قال العلامة ‎ابن عثيمين – رحمه الله – :

Amesema mwanachuoni mkubwa ibn Uthaimin -Allah amrahamu-:

الذي يجعل زوجته بمنزلة الخادم يُهينها ويُتعبها، وربما يخدش كرامتها بسب أبيها وأمها،

Yule ambaye humuweka mkewe katika daraja la mfanya kazi (akawa) anamdhalilisha na kumpa tabu na huwenda akaitia dosari heshima yake kwa kumtukania baba yake na mama yake,

هذا مُخالف لهدي أبي القاسم ﷺ قولًا وفعلًا.

Huyu (mwenye tabia hii) ni mwenye kwenda kinyume na muongozo wa Abul- Qasim (Mtume) -swala na salamu za Allah zimfikie-kikauli na kimatendo .

📕[ فتح ذي الجلال والإكرام (٥٤٣/٤)

Maelezo ya mfasiri :

Kumnyanyasa mke si katika mwenendo wa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-bali yeye amewausia wanaume waishi kwa wema na wake zao na huu ulikua ni miongoni mwa usia wake Mtume -swala na salamu za Allah -katika hija yake ya kuaga, ama kauli yake Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-:

” فإنما هنَّ عَوانٍ عندكم، “

“Hakika ilivyo hao (wanawake) ni mateka kwenu ” .

رواه الترمذي وقال : حديث حسن صحيح

Maana yake:

Mume atilie umuhimu na pupa katika kumsimamia yale yanayohusu dini yake na dunia yake ni kwa sababu huyo mwanamke yupo chini ya mwanamume, ndiyo maana akafananishwa na mateka na wala haina maana anyanyaswe bali ni wajibu apewe haki zake za kisheria na ndiyo maana Allah amesema:

( وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ )

Na (wanawake) wanayo haki kwa sharia (kufanyiwa na waume zao) kama ile haki iliyo juu yao kuwafanyia waume zao .Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao .

البقرة : ۲۲۸ .

Na hivi ndivyo yalivyokuwa maisha yake Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- pamoja na wakeze -Allah awaridhie – yalikuwa ni maisha ya furaha na raha na kuamiliana nao kwa upole na wala haina maana kuwa asimuadabishe ila kama atamuadabisha basi afuate njia za kisheria, na yamethibiti maneno kutoka kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – :

إنِّي أحرِّجُ حقَّ الضَّعيفينِ : اليتيمِ ، والمرأَةِ

Hakika mimi natahadharisha (kudhulumu) haki za wanyonge wawili : yatima na mwanamke

صحيح الجامع
الرقم ٢٤٤٧

Hii ni tahadhari kutoka kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -juu ya kuwadhulumu wanyonge hawa wawili : Yatima ni mtoto ambaye baba yake amefariki na hali hajabaleghe, na mwanamke pia ni mnyonge kwa maumbile yake na akili yake kwa hiyo mume anatakiwa achunge na atahadhari na kumdhulumu mkewe ambaye yeye amepewa jukumu la kumsimamia

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 28 , 1444H ≈ Oct 24, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *