قال ابن الجوزي رحمه الله تعالى
Amesema ibn Al-jauziy – Allah amrahamu
” من أحب أن لا ينقطع عمله بعد موته فلينشر العلم ”
Mwenye kupenda yasikatike matendo yake baada ya kufa kwake (basi) aeneze Elimu.
التذكرة 55
Attazkirah (55)
Maelezo:
إِنَّا نَحْنُ نُحْىِ ٱلْمَوْتَىٰ وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُواْ وَءَاثَٰرَهُمْ ۚ وَكُلَّ شَىْءٍ أَحْصَيْنَٰهُ فِىٓ إِمَامٍۢ مُّبِينٍۢ
Hakika sisi tunawafufua maiti na tunayaandika waliyo yatanguliza na waliyo yaacha (nyuma). Na kila kitu tumekidhibiti katika daftari linalobainisha.
Ufafanuzi:
Allah atawafufua waja siku ya kiama na atawalipa juu ya matendo yao waliyoyafanya ya kheri na ya shari. na matendo ya wanadamu yamegawanyika mara mbili:
1 – Kuna yale wanayoyatenda na yakaishia hapo hapo yaani baada ya kufa athari yake si yenye kuendelea kama vile swala, funga n k.
2 – Kuna matendo ambayo athari yake ni yenye kuendelea hata baada ya kufa sawa sawa yawe ya heri au shari ya heri kama vile: Mtoto mwema au matendo ambayo wameyahuisha wao na watu wakawaiga, kama vile kusambaza elimu na mengineyo mengi ambayo athari yake ni yenye kuenea na kuendelea.
Hili tutafafanua zaidi katika makala ya ” yanayomnufaisha muumini baada ya kufa ” Itaandaliwa In Shaa Allah.
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 16 – Safar – 1442H ≈ 03 – October – 2020M.
Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz
Muhimu: Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•