Amesema Allah-aliyetukuka- akielezea yale watakayo yazungumza makafiri siku ya kiama:
” فَمَا لَنَا مِن شَافِعِينَ “
” وَلا صَدِيقٍ حَمِيمٍ“
“Basi hatuna waombezi”
“Wala rafiki khalisi”
الشعراء : (١٠٠ – ١٠١)
Ash-shuaraa (100-101)
قالَ الحسنُ البصْريّ -رحمه الله-:
Amesema Al-hasan Al-baswriy- Allah amrahamu-:
{ اسْتكْثِروا منَ الأصْدِقاءِ المُؤمنِين ؛ فإنّ لهُم شفَاعةً يومَ القيَامة }
Kithirisheni (kuwa na) marafiki waumini ,bila shaka hao (marafiki) wanauombezi siku ya kiama.
📓تفسير البَغَوي (٣٤٠/٨)
Maelezo :
Makafiri watazungumza maneno haya siku ya Kiama pindi watakapowaona Malaika na Manabii na waumini wakiwaombea waislamu ,kwa ajili hii inatakikana muislamu akithirishe kuwa na marafiki wengi waumini ili waje kumuombea siku ya kiama ,na makusudio ya rafiki ni yule aliyekuwa mkweli katika mapenzi ,na kumpata rafiki wa kweli ni nadra haswa katika zama hizi zilizojaa khiana,uwongo n.k.
Kwa ajili hii kumesemwa:
الصديق هو من صدقك،وحدّه : هو مَن فرِح لِفرحك وحزِن لحزنك فهو صديق ومن لا فلا .
Rafiki ni yule aliyekuwa rafiki wako wa kweli, na maana yake : Ni yule anayefurahi kwa furaha yako na anahuzunika kwa huzuni yako (akiwa hivi) basi huyo ni rafiki na yule asiyekuwa hivi si rafiki.
Mwandishi : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 20, 1443H ≈ Dec,24 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•