Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
فضل عشرة ذي الحجة
UBORA WA MASIKU KUMI (10) YA MWANZO YA (MFUNGO TATU) DHUL-HIJJAH 🎤
قال العلامة الفقيه ابن عثيمين- رحمه الله:
Amesema mwanachuoni mkubwa wa fiqih ibn Uthaimin- Allah amrahamu-:
عشرة ذي الحجة تبتدئ من دخول شهر ذي الحجة،
وتنتهي بيوم عيد النحر،
Masiku kumi ya mfungo tatu, yana anza kwa kuingia mwezi wa mfungo tatu,na yanaisha kwa (kuingia) siku ya Eid ya kuchinja (tarehe 10)
والعمل فيها،
قال: رسول الله- صلى الله عليه وسلم-:ما من أيام العمل الصالح فيهن أحب إلى الله من هذه الأيام العشر،قالوا:
ولا الجهاد في سبيل الله؟
قال: ولا الجهاد في سبيل الله،
إلا رجل خرج بنفسه وماله،
فلم يرجع من ذلك بشيئ،
na amali (ibada) katika (masiku) hayo.
Amesema katika hilo Mtume wa Allah- swala na salamu za Allah ziwe juu yake na jamaa zake:
Hakuna katika masiku (ambayo) matendo mema hupendeza zaidi kwa Allah Kuliko masiku haya kumi,
(Maswahaba- Allah awaridhie-) wakauliza:
Hata kuipigania dini ya Allah?
(Mtume) akasema:
Wala kuipigania dini ya Allah,isipokuwa mtu (ambaye) ametoka yeye mwenyewe na mali yake,
na hakikurudi katika hivyo chochote (yaani akafa na mali yake ikateketea).
وعلى هذا فإني أحث إخواني المسلمين على اغتنام هذه الفرصة العظيمة،
وأن يكثروا في عشر ذي الحجة من الأعمال الصالحة،
كقراءة القرآن والذكر بأنواعه،
تكبير، وتهليل، تحميد، وتسبيح،
والصدقة والصيام، وكل والأعمال الصالحة،
na juu ya haya (niliyoyazungumza), mimi nawahimiza ndugu zangu waislamu juu ya kuitumia fursa hii kubwa,na wakithirishe /wazidishe matendo mema katika masiku kumi ya mfungo tatu,kama vile kusoma Qur’ani na nyiradi kwa aina zake (mbalimbali),
kusema Allahu ak’bar, na kusema lailaha illah llah, na kusema Al-hamdulillah, na kusema sub-haana llah,na kutoa sadaqa na kufunga na (kufanya) kila matendo mema ,
والعجب أن الناس غافلون عن هذه العشر، تجدهم في عشر رمضان يجتهدون في العمل،
لكن في عشر ذي الحجة لا تكاد تجد أحدا فرق بينها وبين غيرها،
ولكن إذا قام الإنسان بالعمل الصالح في هذه الأيام العشرة،
إحياء لما أرشد إليه النبي- صلى الله عليه وعلى آله وسلم-
من الأعمال الصالحة، فإنه على خير عظيم .
lakini cha ajabu watu ni wenye kughafilika na (masiku) haya kumi ya (mfungo tatu), utawakuta katika masiku kumi ya (mwisho wa) Ramadhani wakijitahidi katika matendo mema ,lakini katika masiku kumi ya Mfungo tatu unakaribia kutomkuta yeyote anaye tofautisha baina ya (masiku) hayo na mengine yasiyokuwa hayo .
Lakini mwanadamu (muislamu) ataposimama kwa kutenda mema katika masiku haya kumi,
Kwa kuhuisha (muongozo) alioutoa mtume- swala na salamu za Allah zimfikie
(Kwa kufanya) miongoni mwa matendo mema, bila shaka (mtu) huyo yupo katika kheri kubwa.
📚 المصدر: مجموع فتاوى مجلد (21 ص 37-38)
[ Chanzo: Majmu’u fataawa, juzu ya 21, ukurasa (37-38) ]
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Iliandaliwa :August 11,2018M Ikarudiwa Dhul-Qaadah 28, 1442H ≈ Jul 8, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•