UBORA WA MWEZI WA MFUNGO NNE (MUHARRAM)

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

UBORA WA MWEZI WA MFUNGO NNE/ MUHARRAM

https://www.youtube.com/channel/UCUnBTDHVqpDov68uo0Nh18w

๐ŸŽค Sheikh Swaalih Fauzaan Al-fauzaan – Allah amuhifadhi,

Bila shaka huu mwezi una ubora, amesema (Mtume) – swala na salamu za Allah zimfukie- :

” Funga bora baada ya Ramadhani (ni funga ya) mwezi wa Allah Muharram /mfungo nne”

Basi inasuniwa ndani yake kukithirisha kufunga na huo (Mfungo nne) pia ni katika miezi mitukufu na huo ni mwezi ambao waliouteua maswahaba katika zama za Umar – Allah amridhie ili uwe mwaka wa mwanzo wa (tarehe ya) kuhama kwa (Mtume), basi huo ni mwezi wenye fadhila (nyingi) na katika fadhila zake kubwa:

Kwamba ndani yake kuna siku ya ‘Ashuraa ambayo ameeleza Mtume – Swala na salamu za Allah zimfikie- :

Kwamba funga yake inafuta (madhambi) ya mwaka uliopita na bila shaka (funga) hiyo aliifunga Musa – Amani iwe juu yake – kwa kumshukuru Allah pindi Allah alipomuangamiza Firauni na watu wake, basi (Musa) akaifunga (siku) hiyo kwa kumshukuru Allah – aliyeshinda na kutukuka – na waliifunga (funga) hiyo Mayahud baada yake,

Na pindi alipofika Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – Madinah hali ya kuwa ni mwenye kuhama akawakuta Mayahudi wakiifunga (funga) hiyo, basi (Mtume) akasema: Ni (funga) ipi hii mnayoifunga? wakasema: Hakika hiyo ni siku (ambayo) Allah alimpa ushindi Musa na watu wake na alimdhalilisha katika (siku) hiyo Firauni na watu wake na hakika Musa – amani iwe juu yake – aliifunga (funga) hiyo na sisi tunaifunga,

Basi akasema (Mtume) – Swala na salamu za Allah zimfikie- :

” Sisi tuna haki zaidi na Musa kuliko nyinyi ” au ” wabora zaidi kwa Musa kuliko nyinyi “

Basi akaifunga (funga) hiyo (Mtume) – swala na salamu za Allah zimfikie – na akaamrisha ifungwe, basi ikawa funga yake ni suna iliyokokotezwa, lakini yeye (Mtume) – swala na salamu za Allah zimfikie – alitutaka tutofautiane na Mayahudi basi akaamrisha (kuanza) kufunga siku moja kabla yake nayo ni siku ya tisa (9) na katika riwaya (nyingine) au ” Fungeni siku moja baada yake lakini funga ya (siku ya) tisa imekokotezwa zaidi,

Basi hufungwa siku hii kwa kuwaiga Manabii wa Allah, Musa – Amani iwe juu yake na Muhammad – swala na salamu za Allah zimfikie – Katika kuifunga (siku) hiyo na hiyo ni siku (ambayo) Allah aliwapa ushindi waislamu kwa mkono wa Musa – Amani iwe juu yake, basi huo ni ushindi kwa waislamu mpaka kitaposima kiama,

Na ni neema kutoka kwa Allah – aliyeshinda na kutukuka – hushukuriwa na hilo ni kwa kufunga, basi funga yake ni suna ya Mtume iliyokokotezwa na muislamu hufunga siku ya tisa na anafunga siku ya kumi (10) ambayo hiyo ndiyo siku ya ‘Ashuraa, na imeendelea suna hii katika umma huu, na sifa zote ni za Allah,

Basi inakokotezwa funga yake kwa kutafuta ujira na thawabu (malipo) na kwa kumshukuru Allah – aliyeshinda na kutukuka.

Kusikiliza sauti ya Sheikh bonyeza link hii: โคต๏ธ
https://youtu.be/V_3WnVM_FAs

Nyongeza ya Mfasiri;

Suna iliyokokotezwa ni ile suna iliyotiliwa nguvu ambayo Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – alidumu nayo au aliihimiza lakini si wajibu.

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: โ˜Ÿ
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: โ˜Ÿ
https://t.me/fawaidussalafiyatz

๐Ÿ—“๏ธ Toleo la kwanza:02-Muharram- 1442H โ‰ˆ21- August – 2020M. Toleo la pili : 2- Muharram-1443H sawa na 10-August-2021M

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     โ€ขโ”ˆโ”ˆโ”ˆโ”ˆโ€ขโœฟโโœฟโ€ขโ”ˆโ”ˆโ”ˆโ”ˆโ€ข

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *