Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
UCHACHE ZAIDI WA ITIKAFU NI PUNDE TU NA WALA SI SAA MOJA !
سئل الشيخ ابن باز -رحمه الله- :
Aliulizwa sheikh ibn Bazi-Allah amrahamu-:
الجلوس في المسجد ساعة هل يسمى اعتكافا ؟
Je kuketi msikitini sehemu ndogo ya muda kunaitwa itikafu ?
فقال :
Basi akajibu:
نعم ، إذا نواه .
Ndio,pindi ataponuia hiyo (itikafu) .
مسائل الامام ابن باز ١٣٦/١
Maelezo ya mfasiri:
Haya ndiyo madhehebu ya wanavyuoni wengi zaidi kwamba muda mfupi zaidi itikafu ni punde nayo ni madhehebu ya Abuu Hanifa ,na Shafiy na Ahmad -Allah awarahamu- kama alivyosema Annawawiy -Allah amrahamu- :
وَأَمَّا أَقَلُّ الاعْتِكَافِ فَالصَّحِيحُ الَّذِي قَطَعَ بِهِ الْجُمْهُورُ أَنَّهُ يُشْتَرَطُ لُبْثٌ فِي الْمَسْجِدِ ,
Na ama uchache zaidi wa itikafu (kauli ) sahihi ambayo wengi zaidi katika wanavyuoni wamekata (kwa kauli) hiyo kwamba kunashurutishwa kuketi msikitini
وَأَنَّهُ يَجُوزُ الْكَثِيرُ مِنْهُ وَالْقَلِيلُ حَتَّى سَاعَةٍ أَوْ لَحْظَةٍ .
Na kwamba inafaa (kuketi muda) mrefu na mchache hata sehemu ndogo ya wakat au punde .
المجموع : ٥١٤/٦
Na miongoni mwa dalili walizotumia ni athari ifuatayo :
عن يعلى بن أمية رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قال :
Kutoka kwa Ya’ala bin Umayyah -Allah amridhie- amesema:
إني لأمكث في المسجد الساعة ، وما أمكث إلا لأعتكف .
Hakika mimi naketi msikitini muda mfupi katika wakati na siketi isipokuwa ili nikae itikafu.
ابن أبي شيبة
Tanbih:
Neno “الساعة” saa unapoliona katika Quran na suna na maneno ya wanachuoni wa kale huwa lina maana ya sehemu katika wakati au muda mdogo katika wakati, na wala halina maana ya saa moja ambayo ina maana ya dakika sitini kwa sababu haya ni matumizi yaliyokuja baadae, na hata hilo jibu la sheikh ibn Bazi-Allah amrahamu-yeye anakusudia sehemu katika muda na wala hakusudii saa moja kwa maana dakika sitini .
Na sasa hivi tukiwa katika kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhani nawausia ndugu zangu waislamu kama tumeshindwa kukaa itikafu kumi lote la mwisho basi tujitahidi kukaa hata kwa muda mfupi kama vile unaposwali adhuhuri ukabakia msikitini mpaka alasiri kwa nia ya itikafu bali unaweza ukaweka nia ya itikafu kwa muda mchache chini ya huo kama ilivyo katika madhehebu yetu ya kishafi uchache wa itikafu ni mtu kuketi msikitini zaidi ya utulivu unaowajibika katika swala kwa maana hata dakika mbili tu na hii ndiyo maana ya kauli yao :
فوق طمأنينة الصلاة .
Ila zingatia kuleta nia pindi unapoingia msikitini weka nia ya kukaa itikafu ,hata ukiingia msikitini kabla ya kukimiwa swala basi weka nia ya itikafu ila usisahau kunuia kwa sababu kanuni ya kisheria inasema:
لا ثواب إلا بنية
Hakuna thawabu isipokuwa kwa nia .
•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa : Ramadhani 23 , 1444H =Apr 13, 2023M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•