قال الشيخ سليمان الرحيلي – حفظه الله-
Amesema sheikh Sulaiman Arruhailiy-Allah amuhifadhi-
عندما تحدث عن عقد السحر :
Pindi alipokuwa akizungumzia vifundo vya uchawi:
وتؤثر في الأبدان،
(Hivi vifundo) vinaathiri katika viwiliwili,
فيخرج أنواعا من الأمراض على البدن،
Na hutoa aina (mbalimbali) miongoni mwa maradhi katika mwili,
وقد يظن أنها أمراض عضوية،
Na huwenda kukadhaniwa kwamba ni maradhi ya viungo,
وهي من السحر،
Na hali (maradhi) hayo yanatokana na uchawi,
حتى ما يسمى بمرض السرطان،
Hata (haya)yanayoitwa maradhi ya saratani (kansa),
فإنه تبين لنا بالتجارب أن من أسباب وقوعه السحر،
Basi hakika hali ilivyo imetubainikia kwa uzoefu kwamba miongoni mwa sababu za kutokea kwake ni uchawi,
وإذا فك السحر،
Na pindi utakapobatilishwa uchawi,
زال هذا المرض بعون الله وتوفيقه.
Huondoka huu ugonjwa kwa msaada wa Allah na taufiqi yake.
📚 شرح كتاب التوحيد (ص ٨.٣-٨.٤)
Maelezo kutoka kwa mfasiri- Allah amuhifadhi:
Analolisema sheikh -Allah amuhifadhi- halina shaka ukirejea kitabu kinachoitwa:
طريق الهداية في درء مخاطر الجن والشياطين علاج العين والسحر والعقم والصرع والسرطان.
[ Kitabu ambacho kimetungwa na Abuu Twilaal Abdul-‘Aziz Al-qahtwaaniy ]
Mwandishi meeleza jinsi gani ugonjwa wa kansa unavyoweza ukawa na mahusiano na masuala ya uchawi! Na yeye ameshawatibia wagonjwa kadhaa na wakapona mpaka madaktari walishangaa na kupigwa na butwaa.
Na hivi karibu kuna ndugu ambaye alikuwa na ugonjwa wa kansa alikuwa akisumbuliwa, lakini aliposomewa Qur’ani hali yake inaendelea vizuri mpaka sasa.
Maana ya vifundo:
Anakusudia vifundo ambavyo wachawi huvifunga na kupulizia pamoja na kusoma visomo visivyofahamika ambavyo ndani yake huwa na majina ya mashetani,
Kila fundo wanapolifunga hupuluzia na hufanya hivi kwa kumkusudia mtu maalumu na huu uchawi huwa unaleta athari kwa aliyerogwa kwa matakwa ya Allah ya kiulimwengu.
Muhimu zaidi kuhusiana na masuala haya ya uchawi ni kumuelekea Allah na kuubatilisha uchawi huo kwa maneno ya Allah (Qur’ani) na sunnah, na wala haifai kuondosha uchawi kwa uchawi kwa sababu huo ni ushirikina.
Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 13, 1443H ≈ Dec 17, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•