UCHUPAJI MIPAKA KATIKA SUNA HII YA MAVAZI!

قال علاء الدين المرداوي الحنبلي – رحمه الله-:

Amesema ‘Alau Ddin Al-mardawi Al-Hanbaliy -Allah amrahamu-:

“يكره أن يكون ثوب الرجل إلى فوق نصف ساقه ، نَصّ عليه ” .

“Inachukiza nguo ya mtu kuwa (fupi) mpaka juu ya nusu ugoko wake ,amelitaja hilo (Ahmad) “

المصدر: الإنصاف: ٣٧٢/١

وقال ابن قاسم الحنبلي -رحمه الله :

” لأن ما فوقه مَجْلَبة لانكشاف العورة غالباً ، وإشهار لنفسه ،

Na amesema ibn Qasim Al-Hanbaliy-Allah amrahamu-:

Kwa sababu kilichokuwa juu ya huo (ugoko) hupelekea kuwa wazi uchi mara nyingi, na kuitangaza nafsi yake ,

ويتأذَّى الساقان بحر أو برد . فينبغي كونه من نصفه إلى الكعب ،
Na hupata maudhi miundi yake miwili kwa joto au baridi basi inatakikana (nguo) iwe nusu yake au isivuke kongo (mbili),

لبعده من النجاسة والزهو والإعجاب ” .

Ili iwe mbali na najisi na kiburi na kujiona.

المصدر: حاشية الروض : ٥٢٨/١

وقال شيخ الإسلام -رحمه الله-:

Amesema sheikh l-islam -Allah amrahamu-:

” ويكره تقصير الثوب الساتر عن نصف الساق ،

Na inachukiza kupunguza nguo yenye kusitiri ikavuka nusu ugoko

قال إسحاق ابن إبراهيم: دخلت على أبي عبد الله وعَلَيَّ قميص قصير أسفل من الركبة وفوق نصف الساق فقال :

Amesema isihaqa bin Ibrahim: (siku moja) niliingia kwa Abuu Abdullah nikiwa na kanzu fupi chini ya magoti na juu ya nusu ugoko, basi akasema:

( إيش هذا ؟ وأنكره . وفي رواية : إيش هذا ؟ لِمَ تُشَهِّر نفسك ؟ )
Kitu gani hichi ? na akampinga .Na katika riwaya (nyingine) :Kitu gani hichi? kwa nini unaitangaza nafsi yako/kwa kutafuta umashuhuri ?

وكذلك لأن النبي صلى الله عليه وسلم قال :

Na hivyo hivyo kwa sababu Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-amesema:

“حَدّ أزرة المؤمن بأنها إلى نصف الساق”، وأمر بذلك ،

” Mpaka wa mavazi ya muumini (mwanamume) ni kufikia nusu ugoko” na akaamrisha hilo,

وفعله في زيادة الكشف تَعْرية لما يشرع ستره ، لاسيما إن فُعل تديناً فإن ذلك تَنَطّع وخروج عن حَدّ السنة واستحباب لما لم يستحبه الشارع ” .

Na kufanya kwake kitendo cha kuzidisha kuuweka wazi (mguu) ni kukiweka wazi kile ambacho ni sheria kukifunika, na haswa likifanywa hilo kwa (sura) ya dini bila shaka huko ni kujikalifisha na kutoka katika mpaka wa sunnah na kulifanya suna lile ambalo Mtume hakulifanya kuwa ni suna

انظر : ( كتاب المسائل ) ص ٨٤، و شرح العمدة ص ٣٦٨

Maelezo ya mwandishi:

Hili ni katika makosa ya kuitekeleza suna hii ya kuvaa nguo nusu ugoko , na wala si suna kuzidisha zaidi ya hapo tena hilo linaweza likapelekea kuonekana mapaja na mapaja ni uchi, au hata kama hayajaonekana mapaja kufanya hivyo ni kuchupa mipaka na katoka katika sunnah! ni pia vazi hilo hupelekea katika vazi la kutafuta umashuhuri na kuoneshewa vidole kila apitapo!

Kinachotakikana nguo ya muislamu mwanamume isifunike kongo mbili za miguu yake, na bora zaidi ifike nusu ya ugoko /muundi wake ama kuzidisha zaidi ya nusu ugoko hiyo si suna bali ni kuchupa mipaka.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 7, 1443H ≈ Feb 8, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *