➡️ makala namba (1)
◾️ السؤال: هل يجور استعمال الأوراق والأقلام والهاتف في العمل للأغراض الشخصية، مع الاستئذان من المدير ؟
Swali:
Je inafaa kutumia Makaratasi na Kalamu na simu za kazini kwa malengo ya mtu binafsi,pamoja na kutaka idhini kutoka kwa mkuu wa kazi ?
◾️جواب العلامة ابن عثيمين رحمه الله:
Jawabu la mwanachuoni mkubwa ibn Uthaimin- Allah amrehemu-:
▫️استعمال الأوراق أو الأقلام الرسمية أو الاتصال بالهاتف على الصفر، فكل هذا لا يجوز،
Kutumia Makaratasi au Kalamu maalum (kwa Ofisi) au kupiga simu (kama vile) nje ya nchi, yote haya hayafai,
فهذا مما أنت مؤتمن عليه، وليس لفلان أو فلان، بل هو للدولة، وإذا كان للدولة فلا يحل لفلان أن يخون فيه،
Hivi (ulivyokabidhiwa) ni katika vile ambavyo wewe umeaminiwa juu yake,na si vya (mtu) fulani au (mtu) fulani,bali ni (mali) ya nchi, na zikiwa ni (mali) za nchi basi haifai (mtu) fulani kufanya hiana ndani yake,
وإذا كان الإنسان يخشى أن يحتاج مثل ذلك للعمل؛ فليحضر من بيته أوراقا وأقلاما خاصة به،
Na akiwa mtu anachelea (kuwa) atavihitajia mfano wa (vitu) hivyo kwa ajili ya kazi (yake binafsi), basi alete kutoka nyumbani kwake (hayo) makaratasi na Kalamu maalum kwa ajili yake.
📚 سؤال على الهاتف (٢ /٦٧٣-٦٧٤).
Maelezo ya mpitiaji:
Haifai kwa mfanya kazi kutumia mali ya ofisi nje ya shughuli za kiofisi sawa sawa iwe ni ofisi ya serikali au isiyokuwa ya serikali ,mfano wa vitu ambavyo watu wengi huzembea na kuvitumia katika shughuli zao binafsi ni kama simu huwenda akatumia simu ya ofisini kwa kuwapigia watu wengine katika shughuli zake na hali salio limejazwa kwa ajili ya shughuli za kiofisi! au akatumia karatasi au kalamu ,na pia gari iliyojazwa mafuta kwa ajili ya shughuli za kiofisi lakini huitumia katika safari zake !, ikiwa ni mali ya serikali haifai kabisa kwa sababu hata huyo mkuu wa kazi hamiliki hilo la kutoa ruhusa ya kutumia mali za serikali, ama zikiwa ni ofisi zisizokuwa za serikali na wahusika wakamruhusu basi kutakuwa hakuna kosa! ,
Na pia kama kutumia kitu kama rula hilo halidhuru kwa sababu ni kitu ambacho hakiteketei kwa kukitumia kama alivyosema sheikh katika sehemu nyingine ,na pia kama vitu havihitajiki kwa maana vitatupwa hakuna ubaya wa kuvichukua kama walivyosema wanavyuoni.
Itaendelea ..Allah akitaka.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 1, 1443H ≈ Jan Feb, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•