UJUMBE KWA WAFANYA KAZI

➡️ makala namba (2)

◾️ قال العلامة ابن عثيمين رحمه الله:

Amesema mwanachuoni mkubwa ibn Uthaimin Allah amrehemu:

ثم لا يحل له أيضا أن يتشاغل بالشيء الخاص لنفسه، مع أن العمل يحتاج إلى التفرغ للوظيفة.

Kisha si halali vilevile kwake (mfanya kazi) kujishughulisha na kitu maalum kwa ajili yake,pamoja na kuwa kazi inamuhitajia
ajishuhulishe na wajibu (fulani).

ولو فرض أن وظيفته فيها فسحة، ويمكن أن يكتب فيها ما شاء أو يطالع ما شاء، فلا بأس،

Na lau kama kutakadiriwa kuwa kazi yake ina muda wa mapumziko,na kukawa kuna uwezekano wa kuandika anachotaka au kusoma anachotaka basi hakuna ubaya,

أما أن يشتغل بأشغاله الخاصة ويدع أعمال الوظيفة فهذا حرام عليه.

Ama akajishuhulisha na shuhuli zake binafsi na akaacha( kufanya) kazi za wajibu (za kiofisi) hivi ni haramu kwake.

والمدير المسؤول لا يملك هذا فيما نعلم، يعني: لا يملك أن يأذن للموظفين الذين عنده أن يستخدموا أدوات الوظيفة.

Na Kiongozi mwenye majukumu (kusimamia) hamiliki hilo kwa vile tunavyojua, nakusudia (kuwa) hamiliki kuwaruhusu wafanya kazi ambao wapo kwake kutumia vifaa vya kazini.

📚 سؤال على الهاتف (٢ /٦٧٣-٦٧٤).

Maelezo ya mpitiaji:

Mfanya kazi haruhusiwi kufanya shughuli zake binafsi wakati wa kazi ila pindi atakapomaliza kazi yake ya wajibu , kama alivyoulizwa hili sheikh ibn Uthaimin -Allah amrahamu- :

Pindi mfanya kazi atakapotekeleza kazi zake alizowajibishiwa na akataka kufaidika katika wakati wa kazi kwa kusoma quran au kusoma chochote chenye faida au hata kama atataka asinzie ili apumzike kidogo ,je anakosa lolote kutokana na hayo (aliyoyafanya) ?

Sheikh akajibu hivi:

” ليس عليه شيء مادام قائما بالعمل الذي وكل إليه ، أما إذا كان يفرط أو ينقص من أداء عمله ، فإن ذلك حرام عليه ولا يجوز ،
Hana kosa lolote madamu ameisimamia kazi ambayo amewajibishiwa ama akiwa anazembea au anafanya mapungufu (katika) kutekeleza kazi zake basi bila shaka hilo ni haramu kwake na haifai,

وأما النعاس فلا رخصة له فيه لأنه لا يملك نفسه فقد ينام عن عمله من حيث لا يشعر “

Ama kusinzia haruhusiwi katika hilo ,kwa sababu yeye haimiliki nafsi yake huwenda akalala (kabisa) akapitwa na kazi bila ya kuhisi.

“فتاوى الحقوق” جمع خالد الجريسي ص ٥٩ .

Nasaha:

Usifanye kazi zako binafsi ndani ya kazi za ofisi ila baada ya kumaliza kazi zako zinazowajibika mahali husika, na tabia hii wanayo hata baadhi ya madaktari utawaona wakichati na hali wagonjwa wamekaa wakiwasubiri wao !wanaofanya hivi watambue kuwa hicho kipato chao kinachoingia katika muda huu ambao ni waofisi lakini wao wanautumia katika mambo yao binafsi ni kipato cha haramu kwa maana hawastahiki kupewa pesa ya muda huo wanaoutumia kwa mambo yao binafsi!.

Itaendelea ..Allah akitaka

Mpitiaji: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 2, 1443H ≈ Feb 3, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *