UJUMBE KWA WAFANYA KAZI

➡️ Makala namba ( 3)

🔴 قال العلامة ابن عثيمين رحمه الله :

Amesema mwanachuoni mkubwa ibn Uthaimin Allah amrehemu:

رواتب الموظفين لا يستحقها الإنسان كاملة إلا إذا أدى العمل كاملا،

Mishahara ya wafanya kazi mtu haistahiki (kupewa) kamili isipokua atakapotekeleza kazi kikamilifu,

فإذا أخلّ بشيء منه فإنه لا يستحق مقابل ما حصل من الخلل ،
Na atakapo acha (kufanya) chochote katika (kazi) basi hakika yeye hastahiki (kupewa mshahara kamili) ili kufidia kile kilichotokea katika uzembe,

💥 ومع الأسف فإن كثيرا من الموظفين الآن لايقومون بما يجب عليهم،

Na kwa masikitiko hakika wengi katika wafanya kazi hivi sasa hawayasimamii yale yanayowajibika juu yao,

⬅️ إما في الزمن بأن لا يحضروا إلا بعد بدء الدوام بما لا يتسامح فيه، أو يخرجوا قبل انتهاء الدوام،

Ima katika muda, kwa kutohudhuria isipokuwa baada ya kuanza muda wa kazi (na hili ni) katika yale ambayo hawaruhusiwi ndani yake, au wakatoka kabla ya kuisha muda wa kazi,

⬅️وإما في العمل بأن يكون في عمله لكنه لا يعطي المراجعين اهتماما ، ولا يعتني بهم،

Na ima katika kazi (utamuona) yuko kazini kwake lakini yeye hawapi umuhimu wale anaowahudumia,na wala hawashughulikii,

⚠️ فهؤلاء لا يستحقون الراتب كاملا ، ولا يستحقون من الراتب إلا بمقدار ما أدوا من العمل

Basi watu hawa hawastahiki mshahara kamili,na wala hawastahiki katika mshahara isipokuwa kwa kiwango ambacho wamekifanyia kazi,

وعلى هذا فيكون ما يأكلونه ويشربونه من هذا الراتب الذي لا يستحقونه يكون- والعياذ بالله- حراما يحاسبون عليه يوم القيامة،

Na juu ya haya (tuliyoyazungumza) kinakuwa kile wanachokula na wanachokunywa kinachotokana na huu mshahara ambao hawaustahiki, unakuwa-tunajikinga kwa Allah- ni haramu watahesabiwa juu yake siku ya Kiama.

📚 التعليق على كتاب القواعد و الأصول الجامعة ص ٢٢٧-٢٢٨

Maelezo ya mpitiaji:

Wafanyakazi /waajiriwa wanaojichelewesha kuingia kazini kwa muda wajue kuwa hawastahiki kupokea mshahara kamili na kama watapokea basi kiwango hicho wasichokifanyia kazi ni haramu kwao kukitumia kwa maana hawastahiki kulipwa sehemu ya huo muda ! , na pia wale ambao hawatekelezi kazi kiukamilifu hukumu yake ni hii hii ! .

Tunamuomba Allah ulinzi na salama .

Inaendelea ..Allah akitaka.

Mpitiaji: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 3, 1443H ≈ Feb 4, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *