➡️ makala namba (4)
🔴 قال العلامة ابن عثيمين رحمه الله تعالى:
Amesema mwanachuoni mkubwa ibn Uthaimin- Allah aliyetukuka amrehemu-:
💥 وقد اشتهر بين الناس أن مال الحكومة مباح ، قالوا لأن ليس له مالك معين ،
Na hakika imeenea baina ya watu kwamba mali za Serikali ni halali (kuzichukua watu) wanasema: Kwa sababu hazina mmiliki maalum,
فيقال إن مال الحكومة هو بيت المال الذي يستحقه جميع الناس،
Basi (watu hawa) huambiwa (kuwa) :Hakika mali za Serikali ndio nyumba/hazina ya mali ambazo zinawastahiki watu wote,
فأنت إذا بخسته فقد بخست كل الناس الذين يستحقون من بيت المال.
Basi wewe utakapopunja (punguza) hakika umewapunja watu wote ambao wanastahiki (kupata chochote) kutoka katika nyumba/hazina ya mali.
◾️ والأعمال نوعان:
🔺 النوع الأول: ميدانية، فيقال افعل كذا وكذا ، فهذا بحسب العمل متى فعله انتهى.
Na kazi zipo za aina mbili:
Aina ya kwanza:
Ni kazi isiyowekewa muda maalumu, huambiwa (mtu) : Fanya kazi kadhaa na kadhaa, basi kazi (kama) hii (muda wake) ni kulingana na kazi (aliyopewa) wakati wowote atakapoifanya (akaimaliza) basi muda wake umeisha.
🔺النوع الثاني : زمنية مقيدة بوقت ، فهذه وإن انتهى العمل الموكول إلى الشخص فإنه يبقى ، فإن وافق الرئيس المباشر على الخروج وكان له الحق فلا بأس.
Aina ya pili:
Ni kazi yenye muda, iliyofungwa na wakati,basi kazi kama hizi hata kama kazi iliyowajibishwa kwa mtu imeisha, hakika yeye (anawajibika) kubakia na kama ataafiki kiongozi anayesimamia utokaji (wa kazini) na akawa na haki (ya kutoka) basi hakuna ubaya
📚 التعليق على كتاب القواعد و الأصول الجامعة ص ٢٢٧-٢٢٨
Maelezo ya mpitiaji:
Haifa kula mali za serikali kwa madai kuwa si mali za mtu maalumu!bali utakuwa umekula mali za ummah, na hata serikali itakuwa si ya kiislamu pia ni haramu kuiibia.
Pia jambo jingine:
Mfanya kazi haruhusiwi kutoka kazini kabla ya muda wa kazi Kuisha ila Kama atakuwa amemaliza kazi yake anayowajibika kuifanya na akapewa ruhusa na mkuu wa kitengo husika.
Na pia kama kazi anayoifanya haiambatani na muda kwa maana anachohitajika kukifanya ni kumaliza kazi yake atakuwa ametimiza wajibu wake, basi katika hali hii akimaliza kazi yake ni ruhusa kuondoka.
Mpitiaji : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 6, 1443H ≈ Feb 7, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•