UJUMBE KWA WALINGANIAJI

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

UJUMBE KWA WALINGANIAJI.

‏قال الشيخ ابن عثيمين – رحمه الله -:

Amesema Shekh ibn Uthaimin -Allah amrehemu-:

‏أيُّها الإخْوةُ، إنَّني أُريدُ مِن كلِّ داعيَةٍ أنْ يَكونَ مُتَخلِّقًا بالأَخْلاقِ الَّتي تَليقُ بالدَّاعيَةِ؛

Enyi ndugu (walinganiaji), hakika mimi nataka kwa kila mlinganiaji awe ni mwenye kujipamba na tabia ambazo zinaendana na mlinganiaji,

حتَّى يَكونَ داعيَةً حقًّا، وحتَّى يَكونَ قولُه أقْربَ إلى القَبولِ.

ili awe mlinganiaji wa kweli,na ili maneno yake yawe karibu zaidi na kukubalika.

‏📚المصدر : زاد الداعية إلى الله

Maelezo:

Walinganiaji yawapasa wawe ni wenye kujipamba na tabia njema ili watu waweze kuikubali da’awa yao,

bali hiyo ni njia yenye athari zaidi ya kulingania kwa sababu watu huathirika zaidi na vitendo kuliko maneno, kama wanavyosema:

الْفِعْلُ أَبْلَغُ مِنَ الْقَوْلِ

Kitendo kinaathari zaidi ya maneno.

Ama mlinganiaji akawa na tabia mbaya Kama vile kujiona, uwongo, khiyana na tabia nyingine zilizokuwa mbaya, bila shaka watu huwenda wasiathirike na kile anachozungumza bali wanaweza wakawa ni sababu ya makafiri kutoingia katika uislamu ,au wanaweza wale waislamu ambao ni wazushi wakaitia kasoro suna /njia ya wema waliopita kutokana na tabia mbaya za baadhi ya walinganiaji

Tunaomba kwa Allah salama

Mpitiaji : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 14, 1443H ≈ Jan 17, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *