UKIFA UTAFUFULIWA

✍🏻 قال بِلال بن سعد -رحمه الله-:

Amesema Bilal ibn Sa’d -Allah amrahamu -:

“يا أهل التقى! إنكم لم تخلقوا للفناء

Enyi wacha Mungu ! hakika nyinyi hamkuumbwa kwa ajili ya kutoweka (kuondoka tu).

وإنما تنقلون من دار إلى دار، كما نقلتم من الأصلاب إلى الأرحام،

Na hakika si vinginevyo (nyinyi) mnahamishwa kutoka nyumba moja kwenda nyumba (nyingine) ,kama mlivyohamishwa kutoka migongoni (mwa baba zenu) kuelekea katika vifuko vya uzazi (vya mama zenu) ,

ومن الأرحام إلى الدنيا، ومن الدنيا إلى القبور،

Na kutoka katika vifuko vya uzazi kuelekea duniani, na kutoka duniani kuelekea makaburini,

ومن القبور إلى الموقف، ومن الموقف إلى الخلود في جنة أو نار”.
Na kutoka makaburini kuelekea (katika) kisimamo (cha Kiama) na kutoka katika kisimamo kuelekea katika (maisha) ya milele peponi au motoni.

📚[سير اعلام النبلاء (٩١/٥)

Maelezo ya mfasiri :

Mwanadamu hakuumbwa ili afe na kutoweka, bali mwanadamu amehamishwa kutoka katika nyumba moja kwenda nyingine kama alivyotaja Bilal ibn Sa’d mpaka pale atapokuja kuingia katika nyumba ya milele siku ya kiama baada ya kufufuliwa, kwa maana fanya uyafanyayo tambua kuwa baada ya kufa utafufuliwa kisha utaingia katika nyumba ya milele kama alivyosema Allah :

{ ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ تُبْعَثُونَ}

{ Kisha hakika nyinyi siku ya Kiama mtafufuliwa }

المؤمنون ١٦

Tanbih :

Wanachuoni wanaeleza kuwa miongoni mwa makosa makubwa ya baadhi ya waislamu ni kuliita kaburi ni nyumba ya milele kwa maana kauli hii inaashiria kana kwamba hakuna kufufuliwa ,bali usahihi ni kuwa kaburini si nyumba ya milele kwa sababu baada ya hapo kuna kufufuliwa kwa hiyo nyumba ya milele ni moto au pepo.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 6, 1443H ≈ Aug 4, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *