Ulazima wa kutingisha midomo miwili na ulimi katika swala na nyiradi na kusoma qurani

(Muwasilishaji swali):

Allah awabariki na Allah awalipe.

Je, inalazimika kutingisha midomo miwili katika swala na nyiradi na kusoma qurani? (Jawabu):

Haiswihi, haziswihi nyiradi wala kusoma quran, ila kwa kutingisha midomo miwili na ulimi. Ama kusoma kwa moyo hakutoshelezi.

Maelezo ya mfasiri:

Unapokuwa unaswali ni lazima usome quran na nyiradi mbalimbali kwa kutingisha ulimi na midomo miwili yaani ni lazima herufi zitamkwe ama ukisoma kwa moyo moyo bila ya kutamka swala hiyo inakuwa haijaswihi yaani ni batili, unapokuwa katika swala ya jamaa unatakiwa utamke kadri ya kutingisha ulimi na midomo miwili na wala usinyanyue sauti mpaka ukamchanganya jirani yako. Vile vile unaposoma qurani nje ya swala na unapoleta nyiradi mbalimbali ni lazima ulimi ucheze na midomo miwili kama ukisoma kwa moyo basi hautozingatiwa kuwa umesoma qurani wala hautazingatiwa umeleta nyiradi.

Mjibuji swali: Sheikh Swaalih Fauzaan Al-fauzaan

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Kiunganishi cha sauti ya Sheikh: https://youtu.be/8gqdDbG087Q

Imeandaliwa: Tarehe 17 – Safar – 1442H ≈ 04 – October – 2020M.

Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz

#Muhimu: Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *