قال ابن القيم – رحمه الله-:
لَوْ شَاءَ رَبُّكَ كُنْتَ أَيْضًا مَثْلَهُمْ …
فالقَلْبُ بَيْنَ أَصَابِعِ الرَّحْمَنِ
Amesema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu-:
Lau Mola wako mlezi angelitaka wewe pia ungekuwa kama wao.
Moyo upo baina ya vidole vya Mwingi wa Rahmah (Allah).
UFAFANUZI:
Ukiwaona watu waovu kama Washirikina,makafiri,waovu katika waislamu wenzako unatakiwa uwatezame kwa macho mawili :
1- Jicho la sheria hili litakufanya uyachukie yale waliyokuwa nayo na kuyabughudhi .
2- Jicho la qadari hili litakufanya uwaonee huruma hao waovu na kumshukuru Allah kwa neema uliyopewa ,na litakufanya uwasitiri waislamu wenzako waliokosea na kutowadhalilisha kwa kuwatangaza!
Tambua kuwa Allah humuongoza amtakaye kwa fadhila zake ,kwa hiyo wewe uliyeongozwa tambua kuwa unaogelea katika fadhila za Allah ,na Allah humpoteza amtakaye kwa maana humuacha kwa kumtompa taufiki ya uongofu kwa uadilifu wake Allah -aliyetukuka-.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 15, 1443H ≈ Oct 11, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•