Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
🎙 قال بعض الحفاظ:
WAMESEMA BAADHI YA WANAVYUONI WAKUBWA WA HADITHI:
رأينا الإمام أحمد نزل إلى السوق بغداد, فاشترى حزمة من الحطب, وجعلها على كتفيه,فلما عرفه الناس, ترك أهل المتاجر متاجرهم, وأهل الدكاكين دكاكينهم, وتوقف المارة في طريقهم,يسلمون عليه ويقولون: نحمل عنك الحطب, فهز بيده ,واحمر وجهه, ودمعت عيناه وقال: نحن قوم مساكين لو لا ستر الله لافتضحنا.
Tulimuona imamu Ahmad ameingia katika soko la Baghdad,(na) akanunua fungu la kuni na kuliweka begani mwake (na) pindi watu walipomjua,wafanya biashara waliacha sehemu zao za biashara na wenye maduka wakaacha maduka yao na wapita njia wakaacha kutembea katikati ya njia zao,(wakawa) wanamsalimia na (huku) wakisema:
Tukubebee kuni,
(basi imam Ahmad) akatingisha mkono wake (ishara ya kukataa) na uso wake ukawa mwekundu na macho yake yakabubujika machozi na akasema:
”Sisi ni watu wanyonge lau bila ya (kuwepo) stara ya Allah tungefedheheka”
📚 MAREJEO:⇣
الحلية (١٨١/٩} لأبي نعيم
Maelezo ya mtarjumu:
Hivi ndivyo wanavyuoni walivyo wanajipamba na sifa ya unyenyekevu na kutopenda kunyanyuliwa ,mfano mwanachuoni mkubwa wa zama hizi ibn Uthaimin- Allah amrahamu- alikuwa hapendi kuitwa “Mwanachuoni mkubwa” na kama mtu atarekodi neno hilo humwambia alifute ,na ilishawahi kutokea mmoja katika vijana alimuomba sheikh asome beti za mashairi alizozitunga katika kumsifu sheikh basi sheikh – Allah amrahamu- alikuwa akimzuia asiendelee mara kwa mara na kumuomba abadilishe maneno ,na kila anaposikia sifa ya kumsifu katika hizo beti humpinga ,basi yule mwanafunzi akasema:
Sheikh hili (la kunikataza) halinufaishi ima nisome au nisisome ,basi sheikh akasema: Nyamaza (usisome hilo) linapendeza zaidi kwangu ,kisha sheikh akazungumza maneno mazito yenye ujumbe wa kipekee nayo ni kauli yake:
لَا تَجْعَلُوا الحقّ مَرْبُوْطًا باِلرِّجَالِ فَالْحَيُّ لَا تُؤْمَنُ عَلَيْهِ الْفِتْنَةُ .
Musiifanye haki kuwa ni yenye kufungwa na watu , kwa sababu aliyekuwa hai hakuaminiki juu yake fitna ” .
Na hii sauti ya kisa hiki imeenea katika mitandao itafute usikilize ndani yake kuna athari kubwa .
Na hivi ndivyo walivyo wanavyuoni wengine kama vile sheikh Al-baniy- Allah amrahamu- na wengine wengi ,kuna mtu mmoja alimpa mualiko sheikh Al-baniy nyumbani kwake na akaitangaza hii ziyara ya sheikh kupitia baadhi vyombo vya habari ,basi walikusanyika watu wengi ili wamuone sheikh na kumsikiliza lakini sheikh alipojua hilo akakataa kwenda na pindi alipoulizwa sababu ya kutokwenda akajibu :
حُبُّ الظُّهُوْرِ يُقَصِّمُ الظُّهُوْرَ
“Kupenda kudhihiri kuna vunja migongo.
Rejea kitabu:
العقيدة أولا لو كانوا
يعلمون ،لأبي إسلام صالح بن طه عبد الواحد ,ج ١،ص ١١-١٢
Maana ya maneno haya:
” Kupenda kudhihiri kunavunja mgongo” .
Mtu mwenye kupenda kudhihiri na kujulikana mwisho wake ni kufedheheka na kudhalilika !
Mtarjumu: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Toleo la kwanza:August 24,2017M , toleo la pili: Mfungo sita 4, 1443H ≈ October 10, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•