UOVU ULIOENEA KUPITIA SIMU !

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

UOVU ULIOENEA
KUPITIA SIMU .

Kurekodi mazungumzo
ya simu bila idhini ya mzungumzaji ni haramu, kwa sababu mazungumzo yanayojiri baina ya mtu na mwenzake ni amana .

قَالَ الْحَسَنُ -رحمه الله- : إِذَا حَدَّثَ الرَّجُلُ الرَّجُلَ بِحَدِيثٍ وَقَالَ: اكْتُمْ عَلَيَّ، فَهِيَ أَمَانَةٌ.

Amesema Al-hasan-Allah amrahamu-:

Pindi mtu atapozungumza na mtu (mwingine) mazungumzo (fulani) ,na akasema: Nifichie (haya maneno) ,basi hiyo ni amana.

رواه ابن أبي شيبة

Na haswa yakiwa mazungumzo ni ya siri na huyo mwenzake akamtaka afiche hiyo siri kwa maneno ya wazi kama vile akamwambia:

“Haya maneno ni baina yangu na wewe “, au anaweza akamtaka mwenzake afiche hiyo siri kwa ishara bila ya kuweka wazi mfano anaweza kumwambia: Je hapa kuna yeyote anayenisikia ? au je upo peke yako ?au akazungumza kwa kunon’gona au akageuka huku na huku.

Kama alivyosema Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- :

إذا حدَّثَ الرجلُ بالحديثِ ثم التفتَ، فهي أمانةٌ.

Pindi mtu atakapo (kusimulia) maneno kisha akageuga (geuka) ,basi hiyo ni amana.

أخرجه أبو داود (٤٨٦٨)، والترمذي (١٩٥٩)، وأحمد (١٤٥١٤)

Kwa hiyo hapa tunajifunza kuwa kurekodi mazungumzo ya simu bila ya mzungumzaji kujua ni katika aina za khiana na hadaa na hila ,na haswa pindi hayo mazungumzo yatakaposambazwa baina ya watu wengine .

Mwisho :

Wamche Allah-aliyetukuka- ambao wanatabia hii ya kuwafanyia khiana waislamu wenzao kwa kuwarekodi bila ya idhini yao , na watambue kuwa khiana ni katika tabia za kinafiki kama alivyosema Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- pindi alipokuwa akizungumzia sifa za mnafiki yaani unafiki wa kimatendo akataja miongoni mwa sifa zake ni :

” وَإِذَا اؤْتُمِنَ خَانَ ‏”

Na anapoaminiwa hufanya khiana” .

Muandishi: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy.

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 10, 1443H ≈ October 16, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *