Upweke wa Allah-aliyetukuka- katika Injili

ذكر في إنجيل مرقس، الإصحاح الثاني عشر، العدد ٢٨-٣٠ قوله:

Kumetajwa katika Injili ya Marko: 12:28 – 30

فجاء واحد من الكتبة وسمعهم يتحاورون فلما رأى أنه أجابهم حسنا سأله أية وصية هي أول الكل. فأجابه يسوع أن أول كل الوصايا هي: اسمع يا إسرائيل الرب إلهنا رب واحد. وتحب الرب إلهك من كل قلبك ومن كل نفسك ومن كل فكرك ومن كل قدرتك. هذه هي الوصية الأولى.

  1. Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamuuliza, katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?
  2. Yesu akamjibu, ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;
  3. Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.

(Marko 12 :28-30)

وكذلك ذكر في الإنجيل نفسه وحدانية الله عندما سأل أحد التلاميذ المسيح – عليه السلام- :

إنجيل مرقس ،الإصحاح ١٢،العدد ٣٢.

” فقال له الكاتب جيدا يا معلم بالحق قلت لأن الله واحد وليس آخر سواه “

Vile vile kumetajwa katika Injili ya Marko hiyo hiyo upweke wa Allah pindi mmoja wa wanafunzi wa Masih – amani iwe juu yake walipomuuliza.

” Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye”

(12: 32)

Maelezo ya muandaaji:

Hii ndio tauhidi yaani upweke wa Mwenyezi mungu – aliyetukuka – ambaye ni Mungu wa Yesu- Amani iwe juu yake – na ni Mungu wa Muhammad- amani iwe juu yake – na Mungu wa mitume wote bali viumbe vyote na mitume wote wamekuja kuufundisha upweke wa Mwenyezi mungu – aliyetukuka -, hakuna Mtume aliyekuja kuwafundisha watu wake kuwa Mungu ni mmoja katika nafsi tatu na wala hakuna Mtume hata mmoja aliyekuja kuwafundisha watu wake kuwa Mungu ana mtoto! na wala Mungu hawezi akawa mtu aliyekuja katika umbile la kibinadamu! Mungu wa kweli ni huyu aliyemuelezea Yesu – Amani imfikie – kuwa yeye ni mpweke hana mshirika na maneno haya yapo katika bibilia ambayo Manaswara ipo mikononi mwao pamoja na kuwa mengi yaliyomo ndani yake yamebadilishwa, na yale yaliyosalia yamefutwa lakini tunatoa dalili hizi kutoka katika vitabu vyao na hii ni dalili kuwa bila shaka huu Unaswara uliopo sasa hivi haukufundishwa na Yesu – Amani imfikie – bali kuna mtu ndiye aliyekuja kuweka mafundisho haya baada ya Yesu – Amani imfikie – kuondoka duniani naye ni Paul ambaye asili alikuwa ni myahudi na huyu alijitokeza baada ya kupita miaka 81 baada ya Isa (Yesu) kunyanyuliwa akabadilisha yale mafundisho ya nabii Isa -amani iwe juu yake-na kuweka mengi yaliyopo ambayo hayakufundishwa na nabii Isa (Yesu) .

Tanbih: Muislamu haruhusiwi kumiliki vitabu hivi vilivyopinduliwa ambavyo vipo kwa Manaswara hivi sasa , na wala haifai kuwepo navyo nyumbani.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 30, 1444H ≈ Dec 24, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *