USIA GHALI KWA WAISLAMU .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

سئل العلامة أحمد النجمي – رحمه الله:-

ALIULIZWA MWANACHUONI MKUBWA AHMAD ANNAJMIY- ALLAH AMRAHAMU -:

بماذا تنصح المسلم في أيامنا هذه ؟

UNAMPA NASAHA ZIPI MUISLAMU KATIKA MASIKU YETU HAYA ?

فأجاب:

AKAJIBU:

أنصح بأن يحيا على التوحيد والعقيدة الصحيحة.

NAMPA NASAHA JUU KUISHI MAISHA YA KUMUABUDU ALLAH PAKEE , NA AISHI JUU YA ITIKADI ILIYOKUWA SAHIHI.

ويعني بأداء الفرائض والواجبات

NAKUSUDIA ATILIE UMUHIMU KUTEKELEZA YALIYOFARADHISHWA NA YA WAJIBU.

والبعد عن المعاصي والمحرمات.

NA KUJITENGA MBALI NA MAOVU NA YALIYOHARAMISHWA.

ومصاحبة الأخيار

NA KUWAFANYA MARAFIKI WATU WEMA.

ومجانبة الأشرار.

NA KUJIEPUSHA NA WAOVU.

ومتابعة السنن.

NA KUFUATA SUNNAH,

ومجانبة البدع.

NA KUJIEPUSHA NA BIDA’A

والحذر من الفتن فهي كثيرة في هذا الزمن.

NA (KUWA) NA TAHADHARI NA FITINA HIZO (FITINA) NI NYINGI ZAMA HIZI.

وأوصيه أن يلزم بيته ويبكي على خطيئته, كما قال النبي – صلى الله عليه وسلم – لأحد أصحابه : ”الزم بيتك , وابك على خطيئتك“

NA NINA MUUSIA AJILAZIMISHE NA NYUMBA YAKE ,NA ALIE JUU YA MAKOSA YAKE, KAMA ALIVYOSEMA MTUME -SWALA NA SALAMU ZIMWENDEE- KUMWAMBIA MOJA YA MASWAHABA WAKE: “JILAZIMISHE (NA) NYUMBA YAKO NA LIA JUU YA MAKOSA YAKO:

المصدر:

📚 فتح الودود ( ١٠٤/١)

MAELEZO YA MTARJUMU :

Sheikh -Allah amrahamu- ametoa nasaha muhimu mno ambazo ufafanuzi wake ni huu :

1- Amemuusia muislamu aishi katika hii dunia hali ya kuwa anamuabudia Allah pekee na hilo halitimii mpaka mtu ajiepushe na ushirikina katika sura zake zote.

Na vile vile anatakiwa muislamu ashikamane na itikadi sahihi ambayo ni itikadi ya wema waliopita.

2- Amemuusia muislamu adumu na kutekeleza yale ambayo Allah amemuajibishia kama vile swala tano n.k ,na kwa mwanamke katika yale aliyowajibishiwa ni kuvaa hijabu.

3- Kujitenga na yale yaliyoharamishwa kama vile ushirikina ,uzinifu ,kula riba,uwongo ,n.k

4- Kuchagua marafiki wema kwa sababu rafiki ana athari kubwa katika maisha ya rafiki yake.

5- Kujiepusha na waovu .

6- Kufuata mwenendo wa Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- kwa sababu yeye ndiye kiigizo chetu .

7- Kujiepusha na bidaa/uzushi na hili halitimii ila kwa kutekeleza sunnah .

Kisha sheikh akatoa usia wa kuwa na tahadhari na fitina ,mabalaa,misukosuko mbalimbali ,na katika njia za kujikinga na fitna ni mtu kujitahidi kudumu na nyumbani kwake na kutochanganyika na watu bila ya sababu ya msingi .

Maana ya kauli yake mtume -Swala na salamu zimwendee-

”الزم بيتك“

“Lazimiana na nyumba yako”

Wanachuoni wetu wanasema kuwa kama kutakuwa na faida ya mtu kutoka nyumbani kwake na kuchanganyika na watu kutokana na elimu aliyokuwa nayo na uwezo wa kuwaathiri watu basi muda huo atawajibika kufanya hivyo, ama yule ambaye hana uwezo huo huyu anatakiwa kulazimiana na nyumba yake na kujiepusha kuchanganyika ovyo na watu ambao watamuathiri na uovu wao, lakini ujumla wa yote mtu anatakiwa asipende kuchanganyika na watu ila kukiwa na maslahi katika hilo .

Mtarjumu: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Tolea la kwanza:January 10,2018M,tolea la pili: Mfungo sita 5, 1443H ≈ October 11, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *