Usia kwa aliyepewa mtihani wa kuangalia mambo ya haramu (machafu)!

Sheikh: Ndio.

(Mfikishaji swali): Allah akufanyieni ihsani – Mtu ambaye amepewa mtihani wa balaa la kutizama (haramu/machafu), vipi atajizuia na balaa hili na hali ya kuwa yeye anapambana na nafsi yake katika hilo?

(Sheikh): Ajiepushe na sehemu zenye fitna (mabalaa) mfano masokoni ambapo ndani yake kuna wanawake na mikusanyiko ya wanawake na kuangalia televisheni ambazo ndani yake kuna wanawake ambao hudhihirisha mapambo yao mbele ya watu. Muislamu wa kike ni wajibu amuogope (amche) Allah na wala asidhihiri katika televisheni kwa sababu wale ambao wanawatizama si wale waliopo pembezoni mwake (tu), (bali) wanamtizama ulimwengu mzima, basi (mwanamke huyu) anaifedhehesha nafsi yake mbele ya huo (ulimwengu mzima). Na yeye (huyo mwanamke) ameamrishwa kujistiri, ameamrishwa kuvaa hijabu, ameamrishwa kujiepusha na machafu! Basi ni wajibu kwa mwanamke wa kiislamu kujilazimisha na hijabu na asidhihiri mbele ya watu hali ya kuwa hajafunika uso wake si katika vyombo vya habari wala si (mahali) pengine.

Mjibuji Swali: Sheikh Swaalih Fauzaan Al-fauzaan

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Kiunganishi cha sauti ya Sheikh: https://youtu.be/Bj9REGRmRak

Imeandaliwa: Tarehe 04 – Safar – 1442H ≈ 21 – September – 2020M.

Kupata faida nyingi tembelea website yetu kwa kubonyeza hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

Usikose kuungana nasi Telegram kwa kubonyeza hapa: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Muhimu: Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *