Usia kwa kila mwanamke aliyeolewa namna ya kuishi na mumewe na haswa wale walioolewa karibuni.

๐ŸŒท ๐ŸŒท
USIA KWA KILA MWANAMKE ALIYEOLEWA NAMNA YA KUISHI NA MUMEWE NA HASWA WALE WALIOOLEWA KARIBUNI

๐ŸŽ™ ู‚ุงู„ ุงู„ุนู„ุงู…ุฉ ุงุจู† ุจุงุฒ ุฑุญู…ู‡ ุงู„ู„ู‡ ุชุนุงู„ู‰ :

Amesema mwanachuoni mkubwa ibn Baz- Allah aliyetukuka amrahamu-:

ู†ูˆุตูŠ ุงู„ุญุฏูŠุซุงุช ุงู„ุนู‡ุฏ ุจุงู„ุฒูˆุงุฌ ุŒ ู†ูˆุตูŠู‡ู† ุจุญุณู† ุงู„ุฎู„ู‚ ูˆ ุทูŠุจ ุงู„ุนุดุฑุฉ ู…ุน ุงู„ุฒูˆุฌ ุŒ

Tunawausia (wanawake) walioingia katika ndoa karibuni ,tunawausia (kushikamana) na tabia njema na kuishi vizuri na mume,

ูˆ ุงู„ุชุญู…ู‘ู„ ู„ู…ุง ูŠู‚ุน ู…ู† ุชู‚ุตูŠุฑ ู…ู† ุงู„ุฒูˆุฌ ุญุชู‰ ุชุณุชู‚ูŠู… ุงู„ุฃุญูˆุงู„ ุŒ ูˆ ุฃู† ุชูƒูˆู† ุญุณู†ุฉ ุงู„ุฃุฎู„ุงู‚ ุŒ ุญุฏูŠุซู‡ุง ู…ุน ุฒูˆุฌู‡ุง ุทูŠู‘ุจ ุŒ

Na kuvumilia yale yanayotokea kama vile mapungufu ya mume ili hali (yao ya ndoa) isimame sawa sawa, na awe mzuri wa tabia , (na) mazungumzo yake na mumewe (yawe) mazuri,

ุชู‚ูˆู… ุจูˆุงุฌุจู‡ุง ููŠ ู…ู†ุฒู„ู‡ุง ุŒ ุชุนุชู†ูŠ ุจู†ูุณู‡ุง ู…ู† ุฌู‡ุฉ ุงู„ู†ุธุงูุฉ ูˆ ุงู„ุทูŠุจ ุŒ ูˆ ุงู„ุญุฏูŠุซ ุงู„ุทูŠู‘ุจ ู…ุน ุฒูˆุฌู‡ุง ุŒ

Atekeleze wajibu wake nyumbani kwake ajitilie umuhimu kama vile katika upande wa usafi na (kutumia) manukato na kuzungumza vizuri na mumewe ,

ู„ุฃู† ู‡ุฐุง ู…ู† ุฃุณุจุงุจ ุซุจุงุช ุงู„ุฒูˆุงุฌ ูˆ ุจู‚ุงุฆู‡ ูˆ ุงุณุชู…ุฑุงุฑู‡ .

Kwa sababu hizi ni katika sababu za kuthibiti ndoa na kubakia na kuendelea.

๐Ÿ‘ˆ ูˆ ู†ุญุฐู‘ูุฑู‡ุง ู…ู† ุงู„ุนู†ู ูˆ ุงู„ุดุฏุฉ ุŒ ุฃูˆ ุนุฏู… ุชู†ููŠุฐ ุฃูˆุงู…ุฑู‡ ุงู„ุชูŠ ู„ุง ู…ุญุฐูˆุฑ ููŠู‡ุง ุŒ ุจู„ ุงู„ู…ุดุฑูˆุน ู„ู‡ุง ุฃู† ุชุนุชู†ูŠ ุจุฃูˆุงู…ุฑู‡ ูˆ ุชู†ูู‘ุฐู‡ุง ู„ู‡ ุฅุฐุง ูƒุงู† ู„ูŠุณ ููŠู‡ุง ู…ุญุฐูˆุฑ ุดุฑุนู‹ุง ุŒ

Na tunamtahadharisha na (kutumia) vurugu na ukali au kutotekeleza maamrisho yake (mume) ambayo hayana uharamu ndani yake ,bali ni sheria atilie umuhimu maamrisho ya (mumewe) na amtekelezee pindi itakapokuwa hakuna lililokatazwa kisheria ndani yake,

ุฃู† ุชูƒูˆู† ุทูŠู‘ุจุฉ ููŠ ุงู„ูƒู„ุงู… ู…ุนู‡ ูˆ ุงู„ุญุฏูŠุซ ุจุงู„ุฅุจุชุณุงู… ูˆ ุงู„ุถุญูƒ ุงู„ู…ู†ุงุณุจ ุŒ ูˆ ุชู†ููŠุฐ ุงู„ุฃูˆุงู…ุฑ ูˆ ุทูŠุจ ุงู„ู…ุนุงุดุฑุฉ ุŒ

(Mke) awe mzuri katika kuzungumza na huyo (mumewe), na kuzungumza kwa kutabasamu na kicheko (kwa) mnasaba (wa mazungumzo) ,na kuyapitisha maamrisho (yake) na kuishi (naye) kwa uzuri ,

ูˆ ุทูŠุจ ุงู„ู…ุฎุงู„ู‚ุฉ ุŒ ู…ุน ุงู„ุชุทูŠุจ ู…ุน ุงู„ู†ุธุงูุฉ ุŒ ู…ุน ุฅูƒุฑุงู…ู‡ ุฃู‡ู„ู‡ ูƒุฃู…ู‡ ูˆ ุฃุฎูˆุงุชู‡ ูˆ ุฃุจูŠู‡ ูˆ ู†ุญูˆ ุฐู„ูƒ ุŒ ูƒู„ ู‡ุฐุง ู†ูˆุตูŠ ุจู‡ ุงู„ุฒูˆุฌุงุช ุงู„ุฌุฏูŠุฏุงุช ูˆ ุบูŠุฑู‡ู†ู‘ .

Na kujipamba na tabia mzuri, pamoja na kujitia manukato na (kudumu na) usafi pamoja na kuwakirimu ndugu zake (mume) kama vile mama yake na dada zake na baba yake na mfano wa hao ,yote haya tunawausia wake wapya na wengineo

๐Ÿ“šใ€ุฏู„ูŠู„ ุงู„ุฒูˆุฌูŠู† / ู„ู„ุนู„ุงู…ุฉ ุงุจู† ุจุงุฒ ุฑุญู…ู‡ ุงู„ู„ู‡

Maelezo ya mfasiri:

Wanausiwa wanawake walioolewa karibuni na hata wale walioolewa zamani pia wawe na tabia mzuri na waishi vizuri na waume zao ,na wavumilie mapungufu ya waume zao kwa sababu kila mwanadamu ni mwenye kukosea kama alivyosema Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie-:

ยซูƒู„ู‘ู ุจู†ูŠ ุขู“ุฏู… ุฎูŽุทู‘ูŽุงุกูŒ, ูˆุฎูŠุฑู ุงู„ุฎูŽุทู‘ูŽุงุฆููŠู†ูŽ ุงู„ุชูˆู‘ูŽุงุจูˆู†ยป

โ€œWanadamu wote ni wenye kukosea na wabora katika wale wenye kukosea ni wenye kutubu ” .

ุฑูˆุงู‡ ุงู„ุชุฑู…ุฐูŠ ูˆุงุจู† ู…ุงุฌู‡ ูˆุงู„ุฏุงุฑู…ูŠ ูˆุฃุญู…ุฏ .

Azungumze na mumewe vizuri,atilie umuhimu majukumu ya nyumbani kwake kama kupika,kufua,kulea familia n.k, na autilie umuhimu mwili wake kwa kuusafisha na kujipaka manukato pindi anapokuwa na mumewe na sheikh akaeleza kuwa mambo haya ni katika sababu za kudumu ndoa .

Tahadhari:

Mwanamke ajitahadharishe na tabia ya kumfanyia vurugu mumewe na kutumia ukali au kutotekeleza maamrisho ya mumewe yasiyopingana na sheria na matendo haya ni katika sababu za kuvunjika ndoa .

Azungumze na mumewe hali ya kutabasamu na kucheka na Mtume- swala na salamu za Allah – anasema:

ยซุชูŽุจูŽุณู‘ูู…ููƒูŽ ูููŠ ูˆูŽุฌู’ู‡ู ุฃูŽุฎููŠูƒูŽ ู„ูŽูƒูŽ ุตูŽุฏูŽู‚ูŽุฉูŒยป

Tabasamu lako katika uso wa ndugu yako kwako ni sadaka .

ุฑูˆุงู‡ ุงู„ุชุฑู…ุฐูŠุŒ ูˆุตุญุญู‡ ุงู„ุฃู„ุจุงู†ูŠ (ุณู†ู† ุงู„ุชุฑู…ุฐูŠุ› ุจุฑู‚ู…: (ูกูฉูฅูฆ).

Ikiwa kutabasamu kwake muislamu katika uso wa ndugu yake muislamu kwake ni sadaka ,je mke kutabasamu katika uso wa mumewe ?! bila shaka ni sadaka na zaidi ya sadaka .Vile vile mke anatakiwa awapende na kuwafanyia wema ndugu wa mume na hili litamfanya mume azidi kumpenda na hata ndugu wa mume pia watampenda

Tanbih: Maneno ya sheikh -Allah amrahamu- yamejirudia rudia sana kwa sababu asili ya haya maneno shekhe aliyazungumza na lugha ya kuzungumza inatofautiana na lugha ya kuandika.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: โ˜Ÿ
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: โ˜Ÿ
https://t.me/fawaidussalafiyatz

๐Ÿ—“๏ธ Imeandaliwa: Mfungo tisa 22, 1443H โ‰ˆ Jan 25 , 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     โ€ขโ”ˆโ”ˆโ”ˆโ”ˆโ€ขโœฟโโœฟโ€ขโ”ˆโ”ˆโ”ˆโ”ˆโ€ข

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *